Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Suala la rushwa na ufisadi ni mambo linalosumbua duniani kote. Rushwa inatikisa katika mataifa mengi ulimwenguni yaliyoendelea na yasiyoendelea na ushahidi unaonyesha kuwa rushwa inaumiza watu maskini kupita kiasi.
Kwa mujibu wa makala iliyotolewa katika tovuti rasmi ya Serikali ya Afrika ya Kusini International Anti-Corruption Day 2022 | South African Government wanaeleza kuwa rushwa inachangia kukosekana kwa utulivu, kuongezeka kwa umaskini na inachochea kushindwa kwa serikali nyingi barani Afrka.
Pamoja na mapambano ya rushwa kuwa makali sehemu zote ulimwenguni lakini takwimu zinaonesha bado kuna tatizo kubwa katika nchi nyingi za Kiafrika
Rushwa na ufisadi bado vilivyoshamiri nchi nyingi za Afrika
Serikali za Afrika, Sekta Binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, Vyombo vya Habari na wananchi duniani kote wanaungana kupambana na Kapambana na ufisadi na rushwa katika sehemu zao.
Pamoja na mapambano hayo Afrika ndilo bara pekee ambalo limeonekana bado kuna kiwango kikubwa cha rushwa na ufisadi katika maeneo yao kama wanavyobainisha Technoloy katika makala yao ya The least and most corrupt African countries.
Chati ifuatayo ilitolewa mwaka 2020 na Taasisi ya Uwazi ya Kimataifa (Transparency International) ikionesha orodha ya mataifa yaliyokithiri kwa Rushwa na Ufisadi na mataifa yenye unafuu katika nchi za Kiafrika kama ifuatavyo:
Chanzo cha Data: Transparency International
Data hizo zilizotolewa Transparency International ziliangalia kiwango cha rushwa katika mataifa mbalimbali ya Afrika. Takwimu zilizopo kwenye chati hiyo zilipimwa kuanzia namba 0 - 100 hivyo nchi zenye namba kubwa zikiashiria kuwa rushwa imekithiri zaidi kuliko zile zenye namba ndogo.
Hali na mapambano ya Rushwa nchini Tanzania mpaka 2021
Takwimu zilizotolewa na Transparency International, Januari 28, 2021, zinaonesha kuwa, Tanzania imepata alama 38/ 100 na kushika nafasi ya 94 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti. Pia soma: Ripoti ya Upambanaji wa rushwa na Ufisadi kimataifa - Tanzania yang'ara
Kulingana na taarifa hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya pili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikitanguliwa na Rwanda iliyopata alama 54;
Chanzo cha data CPI 2020
Picha: Jedwali likionesha Tanzania ikishika nafasi ya pili katika nchi za Afrika Mashariki
Kiwango cha Rushwa na Ufisadi Tanzania ukilinganisha nchi wanachama wa SADC
Tanzania imeshika nafasi ya saba ikitanguliwa na Seychelles iliyopata alama 66, Botswana alama 60, Mauritius alama 53, Namibia alama 51, Afrika Kusini alama 44 na Lesotho alama 41.
Chanzo cha data CPI 2020
Picha: Data zikionesha nafasi ya Tanzania katika kupambana na Rushwa na Ufisadi katika nchi za Jumuiya ya SADC