Rushwa sio shida sana, ila rushwa inawekezwa wapi ndio shida yenyewe

Rushwa sio shida sana, ila rushwa inawekezwa wapi ndio shida yenyewe

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
UNAJUA MADHARA YA KIUCHUMI YA KUWEKEZA NJE YA NCHI?

Nchi za kiafrika zimelalamikiwa mara kwa mara kujihusisha na rushwa na kutumia fedha hizo kuwekeza kwenye makampuni au benki zilizoko nje ya nchi

Rushwa, ipo kila sehemu duniani. Kuna uwezekano mkubwa rushwa kuwa nyingi katika nchi zilizoendelea kuliko nchi zinazoendelea. Rushwa pia ni sababu ya umasikini lakini pia umasikini huimarika zaidi rushwa inapotumiwa kuwekeza nje

Kwenye andiko ‘how socialism underdeveloped africa’ la Robert Anthony Waters amendika kuwa, Rushwa ni bei ya kuishi, corruption is the price for survival. Mtazamo wa rushwa huangaliwa kawaida na wachumi, kama alivyoonyesha Dambisa Moyo kwenye kitabu cha Dead Aid. Rushwa ni survival ndio sababu rushwa ipo kila mahali

Kiuchumi uwekezaji ndio huwa na madhara zaidi kwa raia. Kama viongozi na wasomi wakiiba kodi za wananchi na kwenda kuwekeza nje, maana yake ni kuwa nchini mwao kiwango cha ajira na uwekezaji kitakuwa chini, huku nchi ambazo wameenda kuhifadhi fedha ikipata ajira zaidi kupitia uwekezaji husika

Tuanze na pesa, ambazo ni kodi za wananchi, zikiibwa na kuwekezwa ndani ya nchi, mabenki yatakuwa na ukwasi wa kuweza kukopesha watu na kuwekeza kwenye miradi tofauti tofauti

Zikiwekwa kwenye benki za nje, ni benki za nje zitakuwa na ukwasi na kuweza kuwakopesha au kuwekeza kwa raia wao na wakaendelea kiuchumi

Hivi karibuni Angola imegundua viongozi na wasomi wametengeneza mfumo wao wa kifedha unaoweza kusafirisha mamilioni kwenda nje ya nchi na wameweza kusafirisha takribani $324 milioni

Hali hii inaleta ugumu kwenye maisha ya kila siku ya waafrika kwa kuwa, Ukwasi ni moja kati ya vitu muhimu ili nchi kuweza kufanya uwekezaji

Watu wamekosa imani kwa makampuni ya ndani, walau kununua hisa, wengi hununua hisa zilizokuwa listed London Stock Of Exchange na kwingineko na kuwapa nafasi makampuni ya nje kukua na kuendelea kwa kasi huku makampuni ya ndani yakifa kwa ukosefu wa ukwasi na kusababisha hali ya bara kwa ujumla kuwa ni lenye umasikini uliokithiri

Signed

OEDIPUS
 
Africa si salama kwa matajiri, imagine ukikosana na watawala unaweza kubambikiwa kesi na kufilisiiwa fasta tu. Hivyo ukiwa na pesa bila kujali ni ya rushwa au halali ni bora ukaiwekeza nje kwenye usalama, vinginevyo ukitaka kuiwekeza hapa ukubali kuwanyenyekea akina makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Africa si salama kwa matajiri, imagine ukikosana na watawala unaweza kubambikiwa kesi na kufilisiiwa fasta tu. Hivyo ukiwa na pesa bila kujali ni ya rushwa au halali ni bora ukaiwekeza nje kwenye usalama, vinginevyo ukitaka kuiwekeza hapa ukubali kuwanyenyekea akina makonda

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ndio tatizo kubwa

Tuliaminishwa umasikini ndio uzalendo mtu akiwa tajiri ni adui, upuuzi huu tuliupata kipindi cha cold war
 
Back
Top Bottom