Rushwa Usalama barabarani - Iringa

Rushwa Usalama barabarani - Iringa

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Jana nilikuwa safarini mkoa wa Iringa. Njiani, ukipita Igingilanyi kwa mbele kuna askari polisi wawili walikuwa wanavizia magari yanayokwenda spidi wakiwa wameficha gari yao aina ya spacio.

Nilichoona ni kwamba mabasi yanapita kasi huku wakidondosha pesa. Hii ni aibu. Kuna haja ya kubadilika. Yale magari na mwendo ule yamebeba watu na wasimamizi wa sheria wanaona kawaida.
 
Tolitoa ushauri kuwa check point ziwe rasmi na zifungwe cctv cameras, lakini kwakuwa wahusika wananeemekea kwenye rushwa kamwe hawatalifanya hilo
 
Tolitoa ushauri kuwa check point ziwe rasmi na zifungwe cctv cameras, lakini kwakuwa wahusika wananeemekea kwenye rushwa kamwe hawatalifanya hilo
Sijui tufanyaje ili kuepuka hili. Inakuwa ni kitu cha kawaida kupokea rushwa kwa askari wetu. Hivi haki itatendeka vipi?
 
Rushwa nchi hii haiwezi ondoka
Labda itungwe sheria ya kunyongwa
Mtu akipatikana anatoa/kupokea rushwa

Ova
 
Jana nilikuwa safarini mkoa wa Iringa. Njiani, ukipita Igingilanyi kwa mbele kuna askari polisi wawili walikuwa wanavizia magari yanayokwenda spidi wakiwa wameficha gari yao aina ya spacio.

Nilichoona ni kwamba mabasi yanapita kasi huku wakidondosha pesa. Hii ni aibu. Kuna haja ya kubadilika. Yale magari na mwendo ule yamebeba watu na wasimamizi wa sheria wanaona kawaida.
Uko sahihi kwa 100%! Hiyo barabara ya Dodoma Iringa, Askari wa usalama barabarani wanaendekeza sana vitendo vya rushwa. Na hasa wale wa Mkoa wa Iringa!

Mabasi makubwa yanatembea kwa spidi zaidi ya 50! Lakini hayapigwi tochi! Ila wewe mwenye gari ndogo wakikupiga tu, basi ni lazima uwape elfu 10! Au wakuandikie faini! Hilo eneo lenyewe la Igingilanyi hakuna msongamano wowote ule wa watu! Lakini kibao kinamtaka dereva eti atembee spidi ya 50/kmh!

Wizi mtupu. Jamaa wanaingiza tu mapato kwa njia ya kuwavizia madereva! Bora zikawekwa camera maalumu badala ya hawa wapigaji.
 
Sijui tufanyaje ili kuepuka hili. Inakuwa ni kitu cha kawaida kupokea rushwa kwa askari wetu. Hivi haki itatendeka vipi?
Wapewe maslai ya kibunge awatopokea rushwa
 
Rushwa nchi hii haiwezi ondoka
Labda itungwe sheria ya kunyongwa
Mtu akipatikana anatoa/kupokea rushwa

Ova
Huyo mnyongaji nae atapewa rushwa atatulia.Bongo KILA sheria ni fursa ugeuzwa dili sehemu ya kupigia kipato.Ukiona mtu kahukumiwa kuna mawili either hana pesa au ananyooshwa.
Tajiri kukaa jela ni uzembe wake.
 
Sasa wewe ujifanye unayafata nyuma hayo mabasi unashindana nayo... Ndo utajua hujui [emoji3][emoji3]
 
Sasa wewe ujifanye unayafata nyuma hayo mabasi unashindana nayo... Ndo utajua hujui [emoji3][emoji3]
Hili nilishuhudia kama ulivyosema safari ni ndefu. Tulipita eneo husika tukamkuta askari anagombana na Dereva fulani. Huenda huyo askari ni cha pombe alikuwa anaongea kingereza hovyo hovyo.
 
Sijui tufanyaje ili kuepuka hili. Inakuwa ni kitu cha kawaida kupokea rushwa kwa askari wetu. Hivi haki itatendeka vipi?
Akipatikana IGP mwenye hofu ya Mungu labda haki itatendeka
 
Baada ya Mhe. Magufuli kufa rushwa barabarani imekuwa kero. Kumbe kwenye utawala wa Magufuli walikuwa waoga kiasi. Utawala uuone tatizo hili na uanze kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom