DOKEZO Rushwa ya ngono Chuo Cha SAUT -Tabora yakithiri

DOKEZO Rushwa ya ngono Chuo Cha SAUT -Tabora yakithiri

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umeongea mambo mazito ambayo kimsingi yanahatarisha usalama, ajira na kusababisha taharuki kwa jumuiya yote ya SAUT.

Cha ajabu hujaweka tone la ushahidi. Kuna mambo matatu, aidha mmeshare demu, umefeli au chuki binafsi. Tangu lini Dean akadetermine perfomance yako? Ukifaulu vizuri inawezekanaje ukapewa supplementary/ carry over/ retake?

All in all umefanikiwa kuweka watumishi wa hapo roho juu cz lazima kutakuwa na ufuatiliaji wa ndani.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu, salama?

Hili suala la rushwa ya ngono imezidi chuo cha SAUT tawi la Tabora hadi kufikia mkufunzi kumuhakikishia mwanafunzi asipotoa rushwa ya ngono hatograduate!

Kibaya zaidi kiongozi wa hili suala la kupenda rushwa hii ni Dean of Student ambaye ndio kinara wa penda penda hii! Kuna haja ya mamlaka husika kuingilia kati maana sasa imezidi kwa sasa hapo chuoni.

Kuna haja ya kufanya behavioral modification miongoni mwa wakufunzi hao maana sasa kama hadi mtu anashindwa kuhitimu kisa mkufunzi analazimisha hadi apewe ngono ndo amruhusu sio vyema! This is too much aiseeee
Je, Umefikisha / kuripoti hizo tuhuma katika ofisi zinazohusika chuoni?

Naamini kuwa vyuo vyote vina idara maalumu ambazo zinashughulikia maswala na changamoto za wanafunzi kuanzia; Idara au kitengo husika mwanafunzi anaposoma, kamati za maadili na hata kufikisha kwa uongozi wa juu taaluma na wakuu wa vyuo.

Kama umeripoti na ukupatiwa ufumbuzi / utatuzi wa tatizo lako basi ungalikuja na ushahidi juu ya tuhuma ambazo unamshtumu muhusika ili sasa jamii tuweze kushauri na kusaidia.

Fikra Busara
 
Kama mtu ni msomi wa chuo kikuu na ana akili timamu anashindwaje kuweka mazingira huyo muhusika akamatwe? kuna polisi kuna takukuru kuna vyombo chungu nzima ama vyenyewe viko kwa ajili ya kushughulikia wapinzani tu? mbona UDOM na AIAA waliweza kuwapata hao wakware na wakakamatika? nyie SAUT mnakwama wapi? tatizo linaweza kuwa ni nyinyi wenyewe.
 
Dean of students na eligibility ya ku- graduate wapi na wapi. Huyu si mhadhiri.

Sijaona evidence ya ukubwa wa hilo tatizo hapo hadi useme hilo tatizo limezidi.
Hata mimi nimeshangaa! Den of Students mbona ni mtu mdogo sana chuoni! Mtoa mada amejikita kwenye kulialia tu, kana kwamba wanaosoma kwenye hicho chuo ni watoto wadogo.

Wanashindwa nini kuchukua hatua madhubuti, ili kukomesha hilo tatizo? Vipi hao wahanga nao wanachangua kwenye ukuaji wa hilo tatizo? Maana watoto wa siku hizi nao wanapenda sana mteremko! Kamwe hawapendi kujituma.
 
nenda takukuru ripoti weka mtego mnashindwaje kuripoti takukuru
 
Back
Top Bottom