Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya Mwaka 2007; Rushwa ya Ngono ni kitendo anachofanya Mtu mwenye Mamlaka, katika kutekeleza Mamlaka yake kudai Ngono au upendeleo wa aina yoyote kutoka kwa Mtu kama kishawishi cha kumpatia Ajira, Cheo, Haki, Fursa au upendeleo mwingine.
Rushwa ya Ngono inapotolewa sehemu za kazi, au sehemu za kutolea huduma husababisha madhara ikiwemo kukwamisha upatikanaji wa haki, mtendewa kukosa huduma muhimu za kijamii, kuongeza idadi ya wenye maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa.
Vilevile Rushwa ya Ngono inasababisha kudhoofisha nguvu kazi ya Wanawake, kuwakosesha Wanawake na Wasichana kipato binafsi pamoja na kuzorotesha Maendeleo na Uchumi wa Nchi kwa ujumla.