Rushwa ya Ngono sehemu za kazi

Rushwa ya Ngono sehemu za kazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya Mwaka 2007; Rushwa ya Ngono ni kitendo anachofanya Mtu mwenye Mamlaka, katika kutekeleza Mamlaka yake kudai Ngono au upendeleo wa aina yoyote kutoka kwa Mtu kama kishawishi cha kumpatia Ajira, Cheo, Haki, Fursa au upendeleo mwingine.

Rushwa ya Ngono inapotolewa sehemu za kazi, au sehemu za kutolea huduma husababisha madhara ikiwemo kukwamisha upatikanaji wa haki, mtendewa kukosa huduma muhimu za kijamii, kuongeza idadi ya wenye maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa.

Vilevile Rushwa ya Ngono inasababisha kudhoofisha nguvu kazi ya Wanawake, kuwakosesha Wanawake na Wasichana kipato binafsi pamoja na kuzorotesha Maendeleo na Uchumi wa Nchi kwa ujumla.
 
Kitu cha kawaida sana huko makazini kwa mdada/mwanamke kugegedwa na kisha na yeye kupewa u -boss au kazi, na fun enough wengi wao wenyewe ndiyo wanana entertain huo mchezo!
 
mi mwanaume nikiombwa rusha ya ngono na bosi mdada............ntaanzaje kukataa
 
mi mwanaume nikiombwa rusha ya ngono na bosi mdada............ntaanzaje kukataa
Ulishawahi kula tunda kimasikhara?
Moja Kwa Moja Kwa Nabii Riki boy kutoa ushuhuda jinsi boss lady alivyonitendea mambo makuu Mario Mimi!
😁😁😁😁🙌
 
mi mwanaume nikiombwa rusha ya ngono na bosi mdada............ntaanzaje kukataa
niliwahi kumtoroka bosi wangu baada ya kugundua kaniingiza kwenye anga zake na kinachofuata ilikuwa ni kwenda kucheza gameu, alinichukia balaa na kunidharau mbele za wafanyakazi wenzangu
 
Nimeshawishiwa Sana na wadada na wamama kazini wanipe Ila hiyo dhambi sijaishiriki Hadi leo
 
Ngono zipo sana tu sehemu za kazi, inashangaza neno rushwa linapong'ang'anizwa huko mapenzini wakati si muafaka kutumika huko. Rushwa ni kwenye fedha tu, yale ni mapenzi, mtu anaomba apewe au atoe penzi ili apate upendeleo au huduma fulani. Sasa kama mtoa penzi anavutia kingono kwa nini bosi asichanganyikiwe kwa umbo na sura ya kuvutia kimahaba wakati mwenza wake wa halali hana? Lugha sahihi hapa ni mapenzi sehemu za kazi na maofisini na athari zake
 
Tusindikize na Picha
tapatalk_1637755820902.jpg
 
niliwahi kumtoroka bosi wangu baada ya kugundua kaniingiza kwenye anga zake na kinachofuata ilikuwa ni kwenda kucheza gameu, alinichukia balaa na kunidharau mbele za wafanyakazi wenzangu
itakua ulikua na matatzo mkuu
 
Vilevile Rushwa ya Ngono inasababisha kudhoofisha nguvu kazi ya Wanawake, kuwakosesha Wanawake na Wasichana kipato binafsi pamoja na kuzorotesha Maendeleo na Uchumi wa Nchi kwa ujumla.
Jamani hata kundi la wanawake na wasichana wa"behave", kuanzia, mazungumzo, matendo, na mavazi yao! Watambue wafanyakazi wenzao wa kiume wameumbwa na tamaa za mwili zilizo karibu. Wasiwanyanyase wenzao Wakiume kisaikolojia kwa kuwafanyia vitendo vya kusisimua hashiki zao a kimwili kama kuleta mazungumzo ya KuchoChea kujamiiana, mavazi yanayochochea mavazi hayo, mikao kwenye ofisi inayoongeza mawazo hayo. Nakadhalika.
 
itakua ulikua na matatzo mkuu
huenda nilikuwa na matatizo ya kisaikolojia itakuaje nimgegedue bosi wangu japo alinitoa wasiwawasi kuwa hayo mambo ni kawaida kutendeka makazini, nami ndio kwanza naanza kazi sikujua kama hayo mambo ni kawaida maofisini, ikabidi nitoroke
 
Mfano ukiwa mwalimu msisititizo mkubwa ni marufuku kugegedua wanafunzi, ila kwa walimu na wafanyakazi wengine ofisini hakuna katazo. Unashangaa binti mdogo anayeanza kazi anajibebisha kwa mzee bosi anayehesabu siku za kustaafu ili apate upendeleo wa kupangiwa kituo kizuri cha kazi. Sasa hapa mzee anaona mawindo, mwanadigidigi kajileta mwenyewe, binti kanona, mbichibichi, kajaziajazia kila idara, anamremburia bosi, sasa bosi afanyaje hapo? Maofisi kuna vituko sana vya kimapenzi kuliko shuleni na vyuoni
 
Kazi na pesa ni bora kuliko iyo kitu apo katikati
Utakufa funza wadudu na michanga vitaila sasa why usiitoe ukapata kaz au pesa
 
Nyie Akina dada ndio sababu ya ngono rushwa mkibana chupi zenu mtakua mmekomesha ngono za rushwa.
 
Rushwa ya ngono sehemu za kazi ni Janga kubwa sana, wanawake wengi wanadhalalishwa kingono na viongozi wao na kupata upendeleo wa nafasi za juu!!! TAKUKURU wanapaswa wachunguze hii aina ya rushwa sehemu za kazi, maana imekuwa ni jambo la kawaida mwanamke kuqnzisha mahusiano na kiongozi wake ili tu apate upendeleo.
 
Back
Top Bottom