Prime Cabinet Secretary Musalia Mudavadi ameibua mjadala mzito baada ya kufichua kuwa serikali ya Kenya iko kwenye mazungumzo na serikali ya Russia kusaidia kurejesha Wakenya wanaodaiwa kupigana vita upande wa Urusi.
Akizungumza na Citizen TV leo, Mudavadi alisema kuwa hali ni mbaya zaidi kuliko ilivyodhaniwa. “Regretfully, several are dead, wengine wako hospitalini, na wengine wanashikiliwa mateka nchini Ukraine,” alisema.
Serikali ya Urusi imetoa takwimu zikionyesha kuwa ni takriban Wakenya 250 pekee ndio wako katika mikataba ya kijeshi, tofauti na madai yanayosema hadi 1000 wamejiunga. Hii inaleta mkanganyiko mkubwa kuhusu idadi halisi ya vijana wa Kenya walioko vitani.
Hata hivyo, twist mpya imezua hasira: serikali ya Urusi imesema haitatoa fidia yoyote kwa walioumia ama familia za waliopoteza maisha wakiwa kwenye majukumu hayo ya kijeshi. Hii imeacha familia nyingi Kenya zikiwa kwenye hali ya huzuni na kukosa matumaini.
Serikali ya Kenya sasa inakabiliwa na shinikizo la kuwajibika na kuhakikisha Wakenya hao wanarejeshwa nyumbani salama. Swali kuu likibaki: ni nani atawajibika kwa maisha yaliyopotea?
Je, vijana wa Kenya wanauzwa kwa vita vya kigeni bila ulinzi wowote? Mjadala unaendelea…