Russia imeingiza takribani dola bilioni 19 (Sh49.27 trilioni) kutokana na mauzo ya mafuta

Russia imeingiza takribani dola bilioni 19 (Sh49.27 trilioni) kutokana na mauzo ya mafuta

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Russia imeingiza takribani dola bilioni 19 (Sh49.27 trilioni) kutokana na mauzo ya mafuta na bidhaa za nishati Machi, ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na miezi ya hivi karibuni ambayo ilikumbwa na kushuka kwa mapato.

Kwa mujibu wa International Energy Agency (IEA), mapato hayo yameongezeka kutoka dola bilioni 9.75 (Sh25.28 trilioni) za Februari, yakionyesha kuimarika kwa sekta ya nishati ya taifa hilo licha ya vikwazo vya kimataifa.

Ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, kufuatia mvutano unaoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, hasa vita vinavyoihusisha Iran.

Soma Pia: Russia kimya kimya anajipakulia minyama $150M kwa siku kutokana na mafuta

Ripoti hiyo inaeleza kuwa pamoja na kupanda kwa bei, Russia pia imeongeza kiwango cha mauzo yake ya mafuta ghafi, ambapo usafirishaji ulifikia wastani wa mapipa milioni 4.6 kwa siku Machi, ukichangiwa zaidi na usafirishaji wa baharini.

Hali hiyo imeiwezesha Russia kufidia hasara iliyotokana na vikwazo vya kiuchumi na changamoto za miundombinu ya nishati zilizokumba sekta hiyo katika miezi iliyopita.

Screenshot 2026-04-14 182320.png
 
Haya sawa mujahedeen lakini Tanzania yenu yenyewe imefaidika na nini katika muktadha mpana huo.
 
Back
Top Bottom