Kama ni kweli, basi hii vita imenishangaza sana huku ikinipa tafakuli kuhusu Rwanda......
Hakuna ukweli wa aina yoyote ni propaganda.
Vyombo vya habari vya magharibi havikuwahi kuizungumzia vizuri Russia kabla ya vita kama havikuwahi kuizungumzia vizuri Afrika kwenye vyombo vyao vya habari; njaa, ukame na vita ndivyo ambavyo Afrika itazungumziwa. Kama ambavyo haikuwahi kuzungumziwa vizuri China.
Ikiwa kama ni mfuatiliaji mzuri wa kinachoendélea Ukraine (binafsi naaangalia Sky news) sikuwahi kuona wachambuzi wa huu mgogoro wakizungumzia kushindwa kwa Ukraine. Kila hatua ambayo Ukraine akiifanya wachambuzi wa kimagharibi waliichambua kama mbinu ya kivita mpaka Ukraine kwa sasa 30% imepokwa na Russia. Ikafika hatua mpaka wachangiaji maoni (comments) wakawa wanahoji: Taarifa wanayopatiwa Ukraine inamdhibiti Russia ipasavyo, imekuwaje 30% ya nchi ya Ukraine ipo mikononi mwa Russia? Hivyo, hivi vyombo vya habari ni zana na wenzetu wanavitumia kwa maslahi yao ijapokuwa kwenye uhalisia ikiwa ni tofauti kabisa.
Russia ilitangaza inafanya SMO. Operation ya kijeshi inakuwa limited baadhi ya vitu havitakiwi kufanywa ikiwemo ni kushambulia miundombinu ya nchi husika ambapo operation hiyo inatendeka. Kilichofanywa na Russia ni kavuka mpaka wa kanuni alizojiwekea mwenyewe. Kwa juzi ameshambulia miundombinu ya umeme, maji na sehemu nyengine amepoteza uwezo wa Internet nchini Ukraine.
Hii inatupatia taswira gani? Inategemea kanuni na sheria za nchi husika military operation zina ngazi ngapi mpaka itangazwe vita kamili. Ikifikia hii hatua ubinadamu unaoonekana kwenye hii SMO unatoweka na kuwa maangamizo hata Ikulu ikalipuliwa. Na ndicho ambacho kinachoonekana kwa Russia inachokifanya. Na hii inatokana na msaada wa kijeshi anaopatiwa Ukraine kwa maana kadri ya kasi ya mashambulizi atakayoifanya dhidi ya Russia kwa Russia inakuwa ni funguo ya kutengua kihunzi cha sheria nchini mwao! Kwa sababu hatokubali apoteze wanajeshi kizembe! Na ndicho kinachoonekana SMO kidogo kidogo inapaa na pengine kwa Russia wanaweza wakatangaza ni vita kamili. Ikifikia hii hatua Russia atatumia nguvu yake yote ya kijeshi.
Tukumbuke kwenye hii operation watafiti wa masuala ya kivita wanasema Russia imetumia 15% ya nguvu yake. Kwa takwimu za kidunia US ni wa kwanza na nguvu yake unaijua. UK, France, German nguvu zao za kijeshi zinafahamika ni kubwa na inafahamika moja ya hio nchi ikiingia vitani inafahamika ni uharibifu wanamna gani utakaoufanya! Lakini takwimu za kidunia zinasema Russia kinguvu ya kijeshi ni ya 2 nyuma ya US. Kwa maana hiyo UK, France, German n.k zinasubiri. Jumlisha na kuwa 15% ya nguvu ya kijeshi ya Russia ndiyo inayotumika Ukraine, akiamua kutumia nguvu zake zote itakuwaje?
50% ya nchi ya Ukraine ipo gizani. Wanakuja baadhi ya watu kwa taarifa ya kuwa 80% ya mitambo imeshafanyiwa ukarabati. Ni suala la kujiuliza tu: Ukraine asilimia kubwa ya shughuli za kiuchumi zimesimama. Punde inataka kutangazwa ni nchi iliyofilisika. Na kitu kikilipuliwa hususani na kombora inafahamika itakuwa kwenye mazingira gani! Shughuli za kiuchum zimesimama! Mtambo mzima watautolea wapi! Au spare parts watazitolea wapi? Video ya kilichotokea kwenye mitambo yao ipo wazi! Imehaaribika kabisa! Ukijiuliza zaidi maswali ni mengi kuliko majawabu! Uzi huu unasema Russia imerusha makombora ambayo 2 au 3 ndiyo yamefanikiwa kupenya kwenye anga ya Ukraine lakini vinu vya kuzalishia umeme vipo maeneo zaidi ya 3. Imekuwaje nusu ya nchi iwe gizani? Ukitafakari hivi unapata maswali mengi kuliko majawabu! Mwisho wa siku inaleta dhana ya kuwa hizi data zinazotolewa kwa manufaa ya Ukraine ni za kupikwa! Ijapokuwa neno hili miongoni mwa hawapendi kulisikia!