Mfaransa Moyoni, Kazini Mbelgiji
Thierry Henry azua hisia mbalimbali
Mnamo 1998, walipoifunga Croatia 2-1 nusu fainali, alikuwa mchezaji wa Ufaransa.
Usiku huu, Thierry Henry, ni naibu mkufunzi wa Ubelgiji na analenga kuiangamiza Ufaransa uwanjani.
Ni mchezaji wa zamani wa Ufaransa aliyekuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 1998.
Mfungaji huyu wa zamani wa Arsenal na Barcelona amesifiwa kwa kuchangia ufanisi wa Red Devils Urusi 2018.
"Thierry Henry ana umuhimu mkubwa kwetu," alinukuliwa beki Toby Alderweireld. "Yeye hutusimulia kuhusu enzi zake akicheza na simulizi hizo hutumotisha.
"Asemalo, huishia kuwa na muhimu na kutufaa. Uwepo wake, uzoefu wake Kombe la Dunia, yote yametupiga jeki Urusi."