Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Roberto Martinez: Mkufunzi wa Ubelgiji mwenye umuhimu mkubwa.
Atawaongoza Red Devils leo wakionana na Ufaransa
Kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez amejizolea sifa kochokocho.

Martinez ameipa Ubelgiji ushindi mechi 19 na kutoka sare mechi 5 ikiwemo ule wa 2-1 dhidi ya Brazil katika robo fainali.

Licha ya kusajiliwa kwa mshangao, miezi mitatu tu baada ya kupigwa kalamu na klabu ya Everton, amekuwa na mchango mkubwa.

Hajawahi kufungwa mechi muhimu tangu achukue usukani Ubelgiji.
 
Mfaransa Moyoni, Kazini Mbelgiji
Thierry Henry azua hisia mbalimbali
Mnamo 1998, walipoifunga Croatia 2-1 nusu fainali, alikuwa mchezaji wa Ufaransa.

Usiku huu, Thierry Henry, ni naibu mkufunzi wa Ubelgiji na analenga kuiangamiza Ufaransa uwanjani.

Ni mchezaji wa zamani wa Ufaransa aliyekuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 1998.

Mfungaji huyu wa zamani wa Arsenal na Barcelona amesifiwa kwa kuchangia ufanisi wa Red Devils Urusi 2018.

"Thierry Henry ana umuhimu mkubwa kwetu," alinukuliwa beki Toby Alderweireld. "Yeye hutusimulia kuhusu enzi zake akicheza na simulizi hizo hutumotisha.

"Asemalo, huishia kuwa na muhimu na kutufaa. Uwepo wake, uzoefu wake Kombe la Dunia, yote yametupiga jeki Urusi."
 
Hugo Lloris apiga mbizi hadi kwenye historia
Kipa wa Ufaransa aweka historia
Hugo Lloris anacheza mechi yake ya 103 timu ya taifa Ufaransa.

Amemfikia mkufunzi wa timu yake Didier Deschamps na kuorodheshwa mchezaji wa sita Ufaransa kuiwakilisha timu ya taifa kipindi kirefu.
 
Nahodha wa Ubelgiji Hazard, tayari amejipa mabao mawili na kuchangia ufungaji wa mengine mawili Kombe la Dunia.

Wachezaji wote wanapenda kukimbia washikapo mpira na kati ya wale waliosalia kwenye Kombe la Dunia, Mbappe (37) na Hazard (30) ndio wanaoongoza kwa idadi ya chenga kamili kufikia sasa.

Alisema haya kuhusu Mbappe:

"Akiwa mdogo alikuwa akitazama video zangu, " Hazard aliiambia RMC Sport. "Kwa sasa, ni kinyume, Ninaheshimu sana mafanikio yake katika umri wake."
 
Back
Top Bottom