Ruti ya DODOMA TO MWANZA - Msaada wa anayejua Kampuni nzuri ya Bus

Ruti ya DODOMA TO MWANZA - Msaada wa anayejua Kampuni nzuri ya Bus

Dr Alfonsi

Member
Joined
Jun 16, 2023
Posts
36
Reaction score
72
Wana familia ya Jf,

Naomba kujuzwa kampuni yenye mabasi mazuri yanayosafiri kuanzia Dodoma mjini kuelekea Mwanza mjini anifahamishe.

Sijawahi kufika Mwanza, ndio mara yangu ya kwanza na safari naanzia hapa Dom mjini.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu mtakao nipa taarifa njema, na pia natanguliza shukrani kwa pisi Kali za Kanda ya ziwa ambazo zitakuwa tayari kunikaribisha jijini mwanza.

ASANTE SANA 🙏
 
Mabasi yapo mengi na yote mazuri. Nenda CBE kwenye booking office zao kata ticket ya basi lolote uanze safari saa 12 asbh ili ufike mapema kwakuwa ni mara ya kwanza.
 
0675 939390 wapigie SATCO Dom Office

Wana usafiri wa kwanza saa kumi na moja alfajiri, Mwanza saa tisa!

Safari njema!

Nauli 35,000/-
 
Chukua SATCO Luxury saa kumi na moja unaondoka.
 
0675 939390 wapigie SATCO Dom Office

Wana usafiri wa kwanza saa kumi na moja alfajiri, Mwanza saa tisa!

Safari njema!

Nauli 35,000/-
Hii namba imekuwa msaada Sana kufanikisha safari yangu... asante mkuu
 
Back
Top Bottom