Kenya 2022 Ruto alaumiwa kurubuni wapinzani

Kenya 2022 Ruto alaumiwa kurubuni wapinzani

Kenya 2022 General Election

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Muungano wa Azimio la Umoja nchini Kenya, uliomsimamisha Raila Odinga kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu, uliofanyika Agosti 9, 2022, umemtuhumu Rais mteule Dk William Ruto kwa kuwarubuni wabunge wake ili waunge mkono muungano wa Kenya Kwanza anaouongoza.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Sektreterieti ya Kampeni za urais za Raila Odinga, Profesa Makau Mutua kupitia taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Agosti 19,2022.

“Tumeshtushwa na taarifa za Naibu Rais William Ruto kujihusisha na vitendo vinavyokiuka utawala wa sheria, Ruto anaendelea kuwarubuni viongozi waliochaguliwa na wagombea binafsi kuhamia upande wake wa Kenya Kwanza,” imeeleza taarifa hiyo.

Profesa Mutua amesema mpaka sasa hakuna mbunge kutoka kwenye muungano wao aliyeamua kuunga mkono Kenya Kwanza kama taarifa zinazozagaa mitandaoni

“Hakuna mwanachama wa Azimio ambaye ameomba kisheria mchakato wa kujiondoa katika muungano wetu. Wanachama wote waliotia saini kama wanachama wa awali bado ni wanachama katika wetu. Kwa hivyo, kasoro zozote zinazodaiwa ni ubatili wa kisheria,” taarifa imeongeza.

Hata hivyo, Azimio la Umoja walioazimia kwenda mahakamani kupinga matokeo ya urais yaliyompa Ruto ushindi, wamesema wana imani watashinda kesi hiyo na nafasi ya urais itarudi kwa mgombea wao Raila Odinga.

MWANANCHI
 
Wapinzani wa EA wanafanana sana kwa tabia zao za kuunga mkono juhudi
 
Makau mutua anajilia tu pesa za Odinga. Alitegemea Odinga akishinda apewe u AG.
 
Back
Top Bottom