Ruto anaenda New York kuleta wawekezaji Rais Samia anaikimbia Chadema yuko Ruvuma

Ruto anaenda New York kuleta wawekezaji Rais Samia anaikimbia Chadema yuko Ruvuma

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Kuna mazuri mengi sana ya demokrasia pamoja na kupigwa watu wanaishi pamoja kwa raha na kujali nchi. Raisi wetu imebidi amtume Majaliwa kwasababu ya kuogopa maandamano huko NY. Mwenzake mfano Ruto wiki chache zimepita ameshaingia mkataba tena na German ambao tuna uhusiano nao wa kupeleka wataalamu 250,000 na kuleta pesa za kigeni na ajira kwa vijana.

Anaenda NY kwenye mkutano na kukutana na wawekezaji. Mama yupo Ruvuma anakimbia Chadema ambao wanaandamana kwasababu ya kukosekana kwa ulinzi watu kutekwa na mpaka kuuliwa mchana kweupe.

Ingekuwa rahisi na manufaa ya nchi kama tungekuwa na katiba nzuri na demokrasia na Raisi afanye kazi za maendeleo na sio kupoteza pesa kuibiwa kura na Polisi, usalama wa nchi kuuwa watu badala ya kulinda na kutusaidia kwenye maslahi ya nchi.

Usalama ungetakiwa badala ya kuwashika viongozi wa Chadema wangetakiwa wawe kule Congo na kufikiria jinsi ya kutafuta masoko ya nchi yetu ubalozini usalama wamejazana ndugu tu kule hawaleti chochote cha kuonekana.

Bila katiba mpya na kujipanga kama nchi huu utaratibu wa sasa wa machawa Watanzania wameuchoka.
 
Mama kafanya kazi kubwa sana, kaimarisha sera za kiuchumi, kaboresha mazingira ya kibiashara na mengine mengi ni muda huu Taifa linanufaika na jitihada zake.

Baada ya kuifungua Tanzania kimataifa sasa hivi ni ziara za mafanikio.
 
acha upotoshaji gentleman,
eti Kenya wapeleke wataalamu 250,000 wapi?🤣

unadanganya mwanzo,
meaning kwamba na hayo mengine ni porojo tu.

by the way,
mambo ya Kenya ama ya Burundi yanayohusu nini Tanzania 🐒
 
Mikataba ya aina hiyo ya ujermani na sisi tulisaini na uarabuni, kiufupi wao wanapeleka madreva, housemaids na kadhalika kama sisi tunavopeleka arabuni, hakuna mkata wewe mwafrika utaingia na mzungu halafu uwe na faida kubwa kwako, german kaona wazee ni wengi viwandani na kazi nyingi za nguvu wakaona waende kenya, ambapo wakenya kwa kazi wanaaminika kuliko wabongo
 
Akienda Ulaya na Marekani mtakuja tena hapa kulia lia , Watanganyika hamuelewi mnataka nini
 
Mama kafanya kazi kubwa sana, kaimarisha sera za kiuchumi, kaboresha mazingira ya kibiashara na mengine mengi ni muda huu Taifa linanufaika na jitihada zake.

Baada ya kuifungua Tanzania kimataifa sasa hivi ni ziara za mafanikio.
Mkuu Tanzania ilikua imefungwa wapi? Imefungukiwa wapi? Imefunguliwa kwa msamaha ama kwa kumaliza kigungo? Ilifungwa lini?
 
Dr Tulia PhD na PM Majaliwa PAMOJA na Mzee Kikwete wako UNGA New York wanatosha 🐼
 
Huyu huyu Ruto mtu wa Sound ?!! Nadhani matatizo yetu waafrica ni mental slavery badala ya kuwaza ni vipi tunaweza tukajikwamua kuwa Bara tunaona uwezo wetu ni kwenda kutafuta neema huko nje.... Ifike wakati tuanze kuwaza ni vipi tunaweza kutatua matatizo yetu wenyewe na ikibidi watu wawe wanakuja huku kutafuta misaada..,
 
Ruto amewashika miguu Ford Foundation aliodai walifadhili maandamano ya Gen Z 😂
Huyu huyu Ruto mtu wa Sound ?!! Nadhani matatizo yetu waafrica ni mental slavery badala ya kuwaza ni vipi tunaweza tujikwamua kama Bara tunaona uwezo wetu ni kwenda kutafuta neema huko nje.... Ifike wakati tuanze kuwaza ni vipi tunaweza kutatua matatizo yetu wenyewe na ikibidi watu wawe wanakuja huku kutafuta misaada..,
 
Hahahahaha!
Nyumbu bwana, inaonekana maandamano yao ya jana yameyeyuka pamoja na akili zao ndogo walizokuwa nazo. Kila wanachoongea Sasa kinakiwa kichekesho tu.
 
Back
Top Bottom