Ruto anataka Ksh 300b(Trilion 6 Tsh) zipunguzwe kwenye bajeti ya Serikali

Wanaanzaga hvyo hvyo, mpe miaka miwili tu ndio mtajua rangi yake vizuri
Hawezi kuwa dicteta Kwa Katiba Yao ilivyo.

Katiba mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA ndo suluhisho.

Ameeen
 
Kwa kuongezea tu wapuuzi wote tuhakikishe hawarudi majimboni wala madarakani
 
Unaweza Ku cut budget ikapelekea uchumi kutokukuwa.Mambo ya uchumi ni complicated weka story nzima iliyosababisha Ruto kuchukua uamuzi huo sio unaandika kimbea mbea.
Daily Nation limetoa summary ya vitu vya kupingwa panga, ww unataka mtoa Mada aeleze nn Tena? Au ndiyo kawaida yenu kuwa wavivu wa kuelewa na kumtafuta sababu zisizo na maana.
 
Kwenye economics reccurrent expenditure ni kubwa kuliko development expenditure, ni ngumu Sana development expenditure kuwa kubwa kuliko development expenditure
 
Wanaanzaga hivi, subiri 2 yrs from now, alafu tuone..!!
Anachofanya ruto ndo itakua kama Yale Yale ya magufuli wafanyakazi hawataongezewa mishahara na watu watakua na Hali ngumu sana

Tatizo la Ruto kama lilivyowanasiasa wengi wa Africa na Dunia kote wanatoa ahadi nyingi nzuri na huku hawana chanzo cha uhakika Cha kuongeza revenue itakayo-finance their development agenda
 
Hyo ni danganya toto tu, ngoja aonje utamu wake mwisho atastaafu na kashfa ya uhujumu uchumi
 
Yani uchumi uteteleke kwa kuondoa matumizi ya sio ya lazima selikalini?, fedha hizo si zitaelekezwa kwenye mahitaji au miradi ya maendeleo?
Anaongelea multiplier effect, mfano unaweza zuia mzunguko was pesa Kwa watu wengi (Velocity + Volume) kwa mfano hamna conference mahotelini, hakuna wateja wa ndege, hakuna disposable income kubwa kwa watumishi hivyo hawatanunua viwanja, magari n.k so hayo makampuni yanayotegemea vipato vya serikali Ina maana itabidi wapunguze wafanyakazi, wasiajiri, wafunge ofisi n.k so inazaa tatizo jingine la mzunguko wa pesa na kukosekana kwa ajira!!

JPM alijitahidi kupunguza matumizi but ndio ikaleta mzunguko mdogo sana wa pesa wa kihistoria tokea miaka ya 70. Na wengine wakaanza mlaumu haajiri n.k so kuwepo balance tu lakini sio kama Bajeti ya matumizi ya kawaida ni kosa kiuchumi.

So uchumi ndio upo complicated hivyo kama alivyosema huyo jamaa.
 
Hapana sio kweli, mbona kasema miradi yenye faida ya muda mrefu au capital intensive izuiwe? So Ina maana hiyo billion 300 pengine ni deficit kwenye recurring expenditure so kuliko kuifund kwa mikopo kaona Bora aing'oe tu kupitia supplementary budget.
 
Kwahiyo unataka viongozi wanaobana matumizi alafu hawatengenezi mifumo wala taasisi imara?.Alafu wawe wananunua wapinzani ili wasihojiwe ujinga wao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kabla ya kushusha lawama kwanza jitahidi kulielewa ja.mbo kwa ndani. Watu wengi hawaelewi tofauti kati ya matumizi ya maendeleo na matumizi ya kawaida katika bajeti ya serikali wanaishia kutupa kawama tu kuwa bajeti ya maendeleo ni ndogo na bajeti ya matumizi ya kawaida ni kubwa. Unapojenga shule au hospitali au barabara hiyo ni bajeti ya mqendeleo lakini ukiajiri madaktari, manesi nq wahudumu wengine ili kuoparete hiyo hospitali pesa za mishahara, kununua madawa, kulipia umeme na huduma zingine ili hospitali itoe huduma zinazotarajiwa pesa inayotumika ni bajeti ya kawaida.; vile vile kwa shule na vitu vingine. Kwa ufupi pesa yote ya mishahara, umeme maji makaratasi, kuzoa taka nk ni bajeti ya kawaida. Hivyo ka.mwe bajeti ya maendeleo haiwezi kuwa kubwa kuliko bajeti ya kawaida labda kama unataka uwe na hospitali haina dawa , wahudumu wa afya, umeme nk.

Serikali ikijenga hospitali au shule bila kuajiri watendaji bado mtalaumu halqfu mtu anataka bajeti ya maendeleo iwe kubwa kuliko ile ya kawaida.
 
Aliyekwambia kupunguza bajeti ndio kuleta maendeleo nani? Hapo ni kujikwamua na mzigo wa Madeni kiufupi ni maumivu hayo wanapata Ili wasianguke.
 
TANZANIA HAITAPATA MAENDELEO kama FEDHA ZA MATUMIZI NI NYINGI KULIKO ZA MAENDELEO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…