Kwa maneno ya kisiasa kuwa pato limeongezeka na mkakopa mara dufu?πππππ Umekimbia Kwa sababu unajua fika kabisa kwamba TRA Sasa imetoka 1.5T/M kuja 2.3T/M ndani ya miaka 3
Kwanini hilo lisiwezake?Kwa hiyo unaweza irwkebisha awamu Yako then baada ya marekebisho yake matunda yasionekane awamu ya 5 ila yaje yaonekane awamu ya 6?
Mbona umeongea kitoto sana?
Suala la madini kuleta pesa halihusiani na mitaji peke yake.Mbona husemi kwamba wawekezaji waliogopa kuweka mitaji awamu ya 5 licha ya hayo marekebisho? Mitaji wameleta baada ya Mama ndio maana unaona Madini inaleta pesa.
Sio wawekezaji wakubwa tu ndio waliowekeza,Magufuli aliwainua hadi wachimbaji wadogo wa sekta ya madini.
Hizi zote sio vital projects za kufanya ukope pesa nyingi.Unauliza miradi ipi? Kwani miradi aloyoacha Mwendazake Kuna mradi hata mmja haukuwa wa Mkopo? Na hiyo ndio miradi iliyokula pesa nyingi za mikopo maana yote ilikuwa chini ya 40% .
On top of that Kuna utitiri wa miradi sekta zote Wala sihitaji kutaja mmja mmja tutajaza seva manaa mingine inaendelea na mingine imekamilika labda tuangalie matokeo ,mfano kwenye Elimu hakuna tena Watoto kuingia shule Kwa mafungu kama nyanya Kwa sababu hakuna madarasa.
Samia amejenga Vyuo vya Veta Wilaya 64,Mikoa 3 kote huko havikuwepo.
Mfano wa 3,Samia anajenga Vyuo Vikuu Mikoa yote Tanzania Kwa kupanua vilivyokuwepo na kuanzisha Kampasi Mpya kwenye Mikoa 15 ambayo haikuwahi kuwa na Chuo.
Mfano wa 4,Samia anajenga viwanja vya ndege Mikoa 14 ambayo haikuwa na viwanja,kupanua na kukarabati vya zamani eg Sumbawanga,Tabora,Kigoma nk nk
Mfano wa 5,Samia anajenga skimu za Umwagiliaji takribani 750 Nchi nzima Zenye hactares zaidi ya 500k
Mfano wa 6,Samia anajenga Barabara BRT huko Dar,Tactic Miji 14 na Kila Mji Kwa Sasa una lami Kwa sababu Bajeti ya Tarura imeongezwa kutoka 294bpn Hadi 850bln ,nk nk
Hapo sijazungumzia Afya,maji na umeme ambako mapinduzi makubwa yamefanyika na yanaendelea Kufanyika.
Hiyo miradi ya Magufuli angekua mwenyewe angeiendeleza pasi na mikopo mingi kama mama yako kizimkazi.