Sasa hapo anaonyesha mfano mbaya kwa Taifa lake.maana kushindwa kuheshimu na kuamini mahakama za nchini mwake anatoa mwanya kwa watu wengi zaidi na maafisa wengi zaidi wa serikali yake na matajiri wengi na wenye pesa zao kufanya maamuzi bila hofu wala uoga kwa kutambua kuwa hata hukumu ikitoka basi hawataiheshimu .
Lakini pia hakuna muwekezaji anayeweza kupenda kuwekeza mahali ambapo mihimili kama mahakama haiheshimiwi.kauli hiyo maana yake inawakimbiza wawekezaji na kuwakosesha imani kwa mifumo ya ndani ya utoaji haki kama vile mahakama. maana yake anataka yeye ndiye kuwa mahakama mwenyewe na muamuzi mwenyewe.jambo ambalo kwa wenye akili hawawezi kuliunga mkono maana anataka kuendesha nchi kibabe kama nyampara.
Pia kauli hiyo inaweza kuchochea Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi kwa kutambua kuwa maamuzi ya mahakama hayaheshimiwi na yanaweza kupuuzwa na kutupiliwa mbali na hivyo dawa ni kumalizana tu.
Kama anaona wananchi ndio watoa haki basi asimamishe mfumo wa mahakama ili kesi zote na mashitaka yote yawe yanapelekwa kwa wananchi wasio juwa hata vifungu vya sheria.lakini pia kauli hiyo ni shambulizi dhidi ya mahakama na mifumo yote ya utoaji haki.
Lakini pia kauli hiyo itawaumiza zaidi wanyonge na maskini kwa kukosa kimbilio la kupata haki zao,hasa pale kesi inapokuwa inawahusu wakubwa na wenye pesa zao au matajiri kwa kuwa watazichezea na kuzidharau hukumu na amri za mahakama na hivyo kuwafanya masikini kuishi kwa kukata Tamaa huku mioyo yao ikiwa inabubujikwa na machozi kwa kukosa mahali pa kukimbilia.jambo Ambalo Ni la hatari sana kwa usalama wa Taifa na utulivu maana watu wanaweza kuingia barabarani kwa kujitoa mhanga bila uoga kwa kusema bora kifo cha heshima cha kupigania haki zao kuliko kuishi kwa mateso ya kuonewa na kudhulumiwa haki zao.