Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 222
- 1,827
Rais William Ruto ametangaza kuwa bei ya unga wa mahindi itashuka zaidi kuanzia wiki ijayo.
Akizungumza katika Kaunti ya Meru leo Jumamosi, Rais Ruto alisema utawala wake umejitolea kusambaza unga wa bei nafuu kwa Wakenya, pamoja na kutokomeza umaskini na njaa.
Alisema licha ya kufika ofisini wakati bei ya unga iliripotiwa kuwa Ksh.230, serikali yake sasa imeweza kuishusha hadi Ksh.170 tayari, na sasa imejitolea kuishusha zaidi hadi Ksh.150 na chini.
“Tulikuta bei ya unga ikiwa Ksh.230, sahii by last week ilifika Ksh.170, tukienda mbele mtaona bei tofauti tofauti…Ksh.150 ikiteremka…kwa sababu tunataka kuhakikisha ya kwamba kila Mkenya anaweza kulisha familia yake na ajisimamie, tuondoea aibu ya njaa katika taifa letu,” alisema.
“Nawashukuru wakulima wengi wa Kenya, niliwaeleza tutawapatia mbegu…sasa tumesambaza mbegu karibu magunia milioni nne katika sehemu mbali mbali. Na mimi nafurahi ya kwamba safari ya kupunguza gharama ya maisha imeanza, na safari ya kupunguza bei ya vyakula imeanza, na mtaona mambo wakati tunaendelea." aliongeza.