Ruvuma: Amchoma mkewe tumboni kisha kunywa sumu baada ya kugundua anatumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI

Ruvuma: Amchoma mkewe tumboni kisha kunywa sumu baada ya kugundua anatumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Tingi, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, kwa tuhuma za kumchoma mke wake tumboni kwa kutumia kitu chenye ncha kali baada ya kugundua kuwa Mke wake alikuwa anatumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV) kwa siri.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema tukio hilo limetokea tarehe 21 Januari 2026 majira ya saa moja usiku katika kijiji cha Tingi.

Amesema kuwa Mtuhumiwa, ambaye jina lake limehifadhiwa, alimjeruhi mke wake baada ya kuzuka ugomvi mkubwa kati yao kufuatia mwanaume huyo kugundua matumizi ya dawa za ARV kwa mke wake bila yeye kufahamu.

Kamanda Chilya ameongeza kuwa baada ya kumchoma mke wake, mtuhumiwa alijaribu kujitoa uhai kwa kunywa sumu.

Wote wawili walikimbizwa katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi, na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
 
Back
Top Bottom