The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia kijana Erick Turuka (23) maarufu kama Keneth, ambaye ni muuza bucha la nyama ya nguruwe, kwa tuhuma za kumuua kikatili msichana wa kazi aitwaye Shukrani Ajiliwa (19), mkazi wa Namihoro, Songea Vijijini.
Akiongea na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma SACP Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea May 15,2025 katika kitongoji cha Namihoro Kijiji Cha Peramiho ambapo Msichana huyo alikutwa amefariki kwa kukabwa shingo na kuchinjwa kwa kitu chenye ncha kali kisha kutobolewa tumbo.
Kamanda Chilya amesema sababu ya kufanya mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Erick kukataliwa kumuoa Shukrani na Wazazi wa Msichana huyo kisha wakamkubalia Mtu mwingine amuoe hivyo kumpandisha hasira Erick na akaona amuue Msichana ili wakose wote.
Jeshi la Polisi limewaasa vijana kujiepusha na hasira za mapenzi na kutochukua sheria mikononi mwao pindi wanapokataliwa, badala yake wakae na subira kwani maisha na upendo havilazimishwi.
Chanzo Nuru FM