The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Aah wapi hii sio kweli. apo lazima bidada KAMLIA VYAKE uyo jamaa.sababu ya kufanya mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Erick kukataliwa kumuoa
Vipi ni athari gani wateja wake wa nyama adhimu wanaipata wakati mtuhumiwa akitumikia kesi yake?Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia kijana Erick Turuka (23) maarufu kama Keneth, ambaye ni muuza bucha la nyama ya nguruwe, kwa tuhuma za kumuua kikatili msichana wa kazi aitwaye Shukrani Ajiliwa (19), mkazi wa Namihoro, Songea Vijijini.
Akiongea na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma SACP Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea May 15,2025 katika kitongoji cha Namihoro Kijiji Cha Peramiho ambapo Msichana huyo alikutwa amefariki kwa kukabwa shingo na kuchinjwa kwa kitu chenye ncha kali kisha kutobolewa tumbo.
Kamanda Chilya amesema sababu ya kufanya mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Erick kukataliwa kumuoa Shukrani na Wazazi wa Msichana huyo kisha wakamkubalia Mtu mwingine amuoe hivyo kumpandisha hasira Erick na akaona amuue Msichana ili wakose wote.
Jeshi la Polisi limewaasa vijana kujiepusha na hasira za mapenzi na kutochukua sheria mikononi mwao pindi wanapokataliwa, badala yake wakae na subira kwani maisha na upendo havilazimishwi.
Chanzo Nuru FM
Kujichukulia sheria mkononi hakuepukiki kama mtaendelea KUKATAA NDOAJeshi la Polisi limewaasa vijana kujiepusha na hasira za mapenzi na kutochukua sheria mikononi mwao pindi wanapokataliwa, badala yake wakae na subira kwani maisha na upendo havilazimishwi.
Unamkatalia mcharanga nguruwe.Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia kijana Erick Turuka (23) maarufu kama Keneth, ambaye ni muuza bucha la nyama ya nguruwe, kwa tuhuma za kumuua kikatili msichana wa kazi aitwaye Shukrani Ajiliwa (19), mkazi wa Namihoro, Songea Vijijini.
Akiongea na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma SACP Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea May 15,2025 katika kitongoji cha Namihoro Kijiji Cha Peramiho ambapo Msichana huyo alikutwa amefariki kwa kukabwa shingo na kuchinjwa kwa kitu chenye ncha kali kisha kutobolewa tumbo.
Kamanda Chilya amesema sababu ya kufanya mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Erick kukataliwa kumuoa Shukrani na Wazazi wa Msichana huyo kisha wakamkubalia Mtu mwingine amuoe hivyo kumpandisha hasira Erick na akaona amuue Msichana ili wakose wote.
Jeshi la Polisi limewaasa vijana kujiepusha na hasira za mapenzi na kutochukua sheria mikononi mwao pindi wanapokataliwa, badala yake wakae na subira kwani maisha na upendo havilazimishwi.
Chanzo Nuru FM
Wao yakiwakumba huwa wanajipiga risasi au kupiga na wenzao wengineMapenzi ukiingia kichwa kichwa ni balaa usione hata polisi wanasema watu wajiepushe na kuacha hasira nao huwa yanawakumba.Poleni na tahadhari zichukuliwe na vijana washauriwe vizuri,haya mambo baba zetu na mababu pia waliyakuta.Kikubwa tahadhari na maelekezo
Kinachoniuma ni mtuhumiwa kuchanganya biashara yake ya kuuza kitimoto na biashara ya mapenziHuyo jamaa hapo ukute alishaanza kuweka vief2 mbili vyake,. Na ukute wakwe vinyama nusu na nini alikua anawazingatia halafu wamekuja kumkataa๐๐๐๐
Inawezekana hata usiwekeze sana ila bado ukaumia parefu sanaMara nyingi hizi so called wivu wa mapenzi ni vijana kuwekeza kwa wanawake vihela vyao vya kudunduliza halafu wanatemwa au kut*mbewa au kuhisi hawathaminiwi.
Wekeza kile ambacho upo tayari kukipoteza!!