Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi mnamo January 02 mwaka huu, wananchi wa Kijiji cha Ng’ombo wilayani Nyasa walimuua mamba na kufanya kitoweo.
Majira ya saa kumi na moja alfajiri kwenye fukwe za Ng’ombo-ziwa Nyasa, Kijiji cha Ng’ombo kata ya Chiwinda, mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Ester Mapunda (48) akiwa anaoga katika fukwe ya ziwa Nyasa alifariki dunia baada ya kukamatwa na mamba kisha kuzama nae majini.
Baada ya tukio hilo wavuvi wa fukwe hizo kwa kushirikiana na askari wa jeshi la polisi na maliasili walifanya msako mkali katika maeneo ya ziwa hilo na kufanikiwa kumuua mamba huyo na wananchi walimfanya kitoweo.