The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia mume na mke, wakazi wa mtaa wa Mji Mwema manispaa ya Songea kwa tuhuma za kuiba mtoto mwenye umri wa miezi 11 (jina limehifadhiwa).
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chillya amesema tukio hilo limetokea Novemba 4, 2024 saa 8:00 mchana.
Kamanda Chillya amesema mtoto huyo ni wa mfanyabiahara wa saluni, Gabriela Hinju (24) ambaye ni kazi wa Mji Mwema manispaa ya Songea.
Kwa mujibu wa Kamanda Chillya, mwanamke huyo alitoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi wilaya ya Songea kuhusu kuibwa kwa mtoto wake.
Gabriela alieleza kwamba siku ya tukio, mwanamke aliyemtambua kwa sura alifika saluni hapo kwa ajili ya kupata huduma ya kusukwa na kipindi yupo kwenye foleni, mtoto wa msusi huyo alikuwa analia ndipo mwanamke huyo akaomba ambebe ili akambembeleze nje, kisha akatokomea naye kusikojulikana.
Kamanda Chillya amesema baada ya tukio, walianza ufuatiliaji mtuhumiwa na mtoto huyo na juzi walimpata mtoto akiwa ndani ya chumba cha fundi cherehani, Janeth Nombo (25) mkazi wa Mji Mwema Manispaa ya Songea anayetuhumiwa kumuiba saluni na kumficha.
“Mtuhumiwa amehojiwa na amekiri kumuiba mtoto huyo akishirikiana na wenzake wawili ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi na kwamba sababu ya kufanya kitendo hicho ni kuwa wameishi na mume wake kwa miaka saba bila kupata mtoto ndipo akaamua kutekeleza azma hiyo ili amdanganye mumewe kuwa amejifungua,” amesema Kamanda Chillya.
Aidha, Kamanda Chillya ametoa wito kwa wazazi na walezi mkoani humo kulinda na kuwatunza watoto na si kuwakabidhi kwa watu wasiowafahamu ili kuepuka matukio ya wizi wa watoto.