DOKEZO Ruvuma: Nguzo za Daraja la Mto Muhuwesi zadaiwa kufikisha miaka minne bila kufanyiwa marekebisho

DOKEZO Ruvuma: Nguzo za Daraja la Mto Muhuwesi zadaiwa kufikisha miaka minne bila kufanyiwa marekebisho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Hizi picha hapa chini zinadaiwa ni za daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Inadaiwa kwamba inakaribia mwaka wa nne sasa tangu nguzo zake zicheze na halijafanyiwa marekebisho hivyo inalazimika gari zote zipite upande mmoja.

======

UPDATES

=======

Ufafanuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ndugu Julius Mtatiro

Julius Mtatiro said:
Ni suala la uelewa tu wa kihandisi. Muhuwesi ni moja ya madaraja yale makubwa kabisa ambayo uhandisi wake ni wa juu na hata gharama za utengenezaji wake ni billions.

Mafuruko ya March 2022 kwenye mto Muhuwesi yalipelekea hili daraja kuhama kidogo kwenye njia yake.

TANROADS ambao ndiyo wasimamizi wa daraja husika walifika kutoka mkoani na Makao Makuu na kufanya tathmini yao - wakaelekeza daraja litumike upande mmoja mpaka pale watakapochukua hatua zaidi.

Kwa mujibu wa Tanroads, daraja ni salama kwa sasa na magari yanaweza kupita kama kawaida lakini wamechukua tahadhari ili kuruhusu magari yapite upande mmoja tu.

Kama kuna maswali au ufafanuzi zaidi ni muhimu mumtafute MD wa TANROAD na timu yao Makao Makuu kwani si rahisi mimi kufahamu kwa undani na kufafanua masuala ya kihandisi.

JSM,
Tunduru,
31 Machi 2023.

=====

HABARI ZAIDI KUTOKA TANROADS;

Nguzo za daraja hazijaathirika wala hazikusogezwa na mafuriko kutoka sehemu moja kwenda nyingine (Daraja lingeanguka).

Kilichoathirika ni sehemu ya juu ya daraja (deck) ambapo nusu ya kwanza ya deck (m 54) ilisukumwa na mafuriko ya maji yaliyokuwa yamebeba magogo kwa takribani sentimeta 20. Deck hiyo ilitembea kupitia bearing zilizo juu ya nguzo za Daraja.


1680219381445.png

1680219407884.png

1680219463788.png
 
Wanasubiri livunjike wapige pesa za ujenzi wa dharura, hapo ni kujichotea mihela mana hakuna ishu ya lpo.
 
Hizi picha hapa chini zinadaiwa ni za daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Inadaiwa kwamba inakaribia mwaka wa nne sasa tangu nguzo zake zicheze...
Hapana mkuu,

Mafuriko yamepita 14/02/2022 ndio yakasababisha hali hiyo.

Mimi nilifika tarehe 15/02/2022 ili kushangaa hali ya pale mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Tunduru alikuwepo pia mheshimiwa Chiza Marando, TANROAD pia walikuwepo kuangalia uharibifu uliotokea.

IMG_20220215_084131_568.jpg
 
Back
Top Bottom