DOKEZO Ruvuma: Nguzo za Daraja la Mto Muhuwesi zadaiwa kufikisha miaka minne bila kufanyiwa marekebisho

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Hizi picha hapa chini zinadaiwa ni za daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Inadaiwa kwamba inakaribia mwaka wa nne sasa tangu nguzo zake zicheze na halijafanyiwa marekebisho hivyo inalazimika gari zote zipite upande mmoja.

======

UPDATES

=======

Ufafanuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ndugu Julius Mtatiro


=====

HABARI ZAIDI KUTOKA TANROADS;

Nguzo za daraja hazijaathirika wala hazikusogezwa na mafuriko kutoka sehemu moja kwenda nyingine (Daraja lingeanguka).

Kilichoathirika ni sehemu ya juu ya daraja (deck) ambapo nusu ya kwanza ya deck (m 54) ilisukumwa na mafuriko ya maji yaliyokuwa yamebeba magogo kwa takribani sentimeta 20. Deck hiyo ilitembea kupitia bearing zilizo juu ya nguzo za Daraja.




 
Duh Nchi ya hatari sana hii!..
Kila sehemu kunavuja...
 
Wanasubiri livunjike wapige pesa za ujenzi wa dharura, hapo ni kujichotea mihela mana hakuna ishu ya lpo.
 
Hizi picha hapa chini zinadaiwa ni za daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Inadaiwa kwamba inakaribia mwaka wa nne sasa tangu nguzo zake zicheze...
Hapana mkuu,

Mafuriko yamepita 14/02/2022 ndio yakasababisha hali hiyo.

Mimi nilifika tarehe 15/02/2022 ili kushangaa hali ya pale mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Tunduru alikuwepo pia mheshimiwa Chiza Marando, TANROAD pia walikuwepo kuangalia uharibifu uliotokea.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…