Ruvuma: Raia wa kigeni akutwa na mashine bandia 60 za dubu

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limetoa taarifa ya kukamatwa kwa mashine bandia 60 za michezo ya kubahatisha pamoja na kumshikilia raia wa kigeni aitwaye Wang Renbiao (28) kwa tuhuma zinazohusiana na tukio hilo.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema kuwa operesheni hiyo ilifanyika Machi 24, 2026 majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Mkuzo, Manispaa ya Songea.

Amesema mtuhumiwa alikamatwa kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi, maafisa wa michezo ya kubahatisha pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwa amehifadhi mashine hizo kwenye stoo kwa lengo la kuzisambaza katika maeneo mbalimbali ya starehe vijijini wilayani Mbinga

Sitasahau 2014 tulipokamatwa kwa tuhuma kama hizo hizo

Kinachofanyika ni michezo ya ndani.. Iko hivi
Sasa hivi kuna wachini wamemonopolize hiyo biashara.. Hakuna mwingine anayeruhusiwa kufanya bali kupitia kwao
Sasa mchina yeyote anayetaka kufanya anawalipa wao kisha wao ndio wanailipa serikali
Akishawalipa wao wanampa lets say mashine 20 zinazotambulika na serikali kwa maana ya kulipiwa kodi.. Halafu anaongezewa nyingine 20 ama zaidi zisizo na stika, kwa maana ya kwamba hizo hazilipiwi kodi
Sasa wana makubaliano kabisa kwamba akikamatwa amalize mwenyewe
 
Kwa kifupi asilimia 90 za hizo mashine hazikidhi viwango na bado asilimia 95 zimechezewa na asilimia 90 hazilipiwi kodi
Hicho kinachoitwa mashine feki ni kwamba hazina stika ya bodi ya bahati na simu lakini hazina tofauti kabisa na zenye stika
 
Aisee huyo mchina wamshughulikie vilivyo.
Anaenda kuwafundisha kamari wakulima, pumbavu sana.
Kama kuna sehemu Watanganyika tunapigwa basi ni kwenye hiyo michezo ya kubahatisha
Kiuhalisia ma shine moja inatakiwa ile 70% na 30% inayobaki ni zawadi za washindi na kodi za serikali.. Lakini nyingi zimechezewa zinakula mpaka 85% na 15 inayobaki ndio zawadi na kodi
 
Sitasahau 2014 tulipokamatwa kwa tuhuma kama hizo hizo

Kinachofanyika ni michezo ya ndani.. Iko hivi
Sasa hivi kuna wachini wamemonopolize hiyo biashara.. Hakuna mwingine anayeruhusiwa kufanya bali kupitia kwao
Sasa mchina yeyote anayetaka kufanya anawalipa wao kisha wao ndio wanailipa serikali
Akishawalipa wao wanampa lets say mashine 20 zinazotambulika na serikali kwa maana ya kulipiwa kodi.. Halafu anaongezewa nyingine 20 ama zaidi zisizo na stika, kwa maana ya kwamba hizo hazilipiwi kodi
Sasa wana makubaliano kabisa kwamba akikamatwa amalize mwenyewe
Mwaka uliopita serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na biashara Selemani Jafo ilitoa waraka wa kupiga marufuku kwa machinga wa kigeni, madalali, mamalishe, babalishe waendesha biashara za "kamari dubwi" na wengine wa aina hiyo.
Cha kushangaza hata baada ya katazo hilo bado tunaona Dubwi za wachina zinaendelea, tatizo nini?
 
Mwaka uliopita serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na biashara Selemani Jafo ilitoa waraka wa kupiga marufuku kwa machinga wa kigeni, madalali, mamalishe, babalishe waendesha wa biashara za "kamari dubwi" na wengine wa aina hiyo.

Akili MTU wangu, jafo alikuwa anafanya siasa TU 😂 aki wadanganya raia
 
Taarifa zinakusanywa vizuri TU, ila viongozi Ndio hawataki kusimamia maslahi ya Nchi, aya bana
 
Kama kuna sehemu Watanganyika tunapigwa basi ni kwenye hiyo michezo ya kubahatisha
Kiuhalisia ma shine moja inatakiwa ile 70% na 30% inayobaki ni zawadi za washindi na kodi za serikali.. Lakini nyingi zimechezewa zinakula mpaka 85% na 15 inayobaki ndio zawadi na kodi
Kutokana na andiko lako hapo juu yaonyesha wewe ni mdau kwenye eneo hilo.
Sisi kama nchi tunakwama wapi kudhibiti ubadhirifu huo?
 
Mwaka uliopita serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na biashara Selemani Jafo ilitoa waraka wa kupiga marufuku kwa machinga wa kigeni, madalali, mamalishe, babalishe waendesha wa biashara za "kamari dubwi" na wengine wa aina hiyo.
Cha kushangaza hata baada ya katazo hilo bado tunaona Dubwi za wachina zinaendelea, tatizo nini?
Tatizo ni moja tuu RUSHWA! na kukosa uzalendo
 
Hii michezo had wabibi wanacheza yaan mambo n ya hovyo kabisa

Kamari za madubwi n hatari sana
 
Sitasahau 2014 tulipokamatwa kwa tuhuma kama hizo hizo

Kinachofanyika ni michezo ya ndani.. Iko hivi
Sasa hivi kuna wachini wamemonopolize hiyo biashara.. Hakuna mwingine anayeruhusiwa kufanya bali kupitia kwao
Sasa mchina yeyote anayetaka kufanya anawalipa wao kisha wao ndio wanailipa serikali
Akishawalipa wao wanampa lets say mashine 20 zinazotambulika na serikali kwa maana ya kulipiwa kodi.. Halafu anaongezewa nyingine 20 ama zaidi zisizo na stika, kwa maana ya kwamba hizo hazilipiwi kodi
Sasa wana makubaliano kabisa kwamba akikamatwa amalize mwenyewe
Na hizi zote zisizo na usajili zinapelekwa kwa wakulima kijijini waliwe pesa za mazao
 
Back
Top Bottom