JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wathirika wa Virusi vya UKIMWI (VVU) wamebainika kutotumia ARV ambazo ni dawa za kufubaza makali ya VVU wanazopewa vituoni kutokana na imani ya dini.
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Mkoani Ruvuma, Josephat Kalipesa amesema hatua hiyo imebainishwa licha ya takwimu za mwaka 2021-2022 kuonesha maambukizi mapya Mkoani Ruvuma ni zaidi ya watu 1,800 sawa na watu watano kuambukizwa kila siku.
Kalipesa ameeleza kuwa kwa jumla ripoti ya maambukizi ya mkoa huo inaonesha idadi ya watu 4,023 sawa na 7% wanadaiwa kuacha kutumia dawa za ARV kutokana na imani ya dini zao.
Amesema: "Kuna wanaotangaza kuwa wamepona ugonjwa wa UKIMWI kutokana na maombi."
Aidha, John Kahimba kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA) anasema aliacha kutumia dawa lakini ndani ya miezi 9 hali yake kiafya ikawa mbaya akalazimika kuanza kutumia dawa za ARV.
Naye, Edmund Kapinga ambaye ni Mwenyekiti wa Waviu Songea anasema wengi walioacha kutumia dawa hizo muda mrefu madhara yalikuwa makubwa na mmoja wao alifariki hivi karibuni.
Source: Azam TV