Ruvuma: Wananchi wa Kata ya Kilagano tunaendea kulima kwenye Hifadhi ya Mlima Lihanje sababu ahadi ya DC ya kutuhamisha imekuwa ‘ahadi hewa’

Ruvuma: Wananchi wa Kata ya Kilagano tunaendea kulima kwenye Hifadhi ya Mlima Lihanje sababu ahadi ya DC ya kutuhamisha imekuwa ‘ahadi hewa’

Joined
Sep 23, 2024
Posts
64
Reaction score
43
screenshot_20241202-165435-png.3172622

Hifadhi ya Mlima Lihanje ni chanzo pia cha maji kwa Wakazi Kata ya Kilagano, Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Pamoja na faida hiyo kuna uharibifu unaoendelea wa kuendesha shughuli za kilimo katika Mlima huo.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile alipotembelea eneo hilo Desemba Mwaka 2023 alijionea kinachoendelea, akatoa maagizo kwa Mwenyekiti wa Kijiji kuwa Wananchi wapewe taarifa ya kutoendelea na shughuli za kilimo katika Hifadhi ya Mlima huo.

Aliahidi kurudi na kufanya mkutano wa hadhara ili kufikia mwafaka wa hifadhi hiyo. Viongozi wa Kata walitekeleza kwa kuwafukuza na kubomolewa kwa nyumba zilizopo pembezoni mwa hifadhi na kubandika vibao vinavyotoa onyo.

Mwaka huu (2024) kweli Mkuu wa Wilaya alirudi katika Kata akiwa na mwafaka wa kuwapa hekari 2,474 waathiriwa waliokuwa wanalima kwenye hifadhi.

Maelekzo hayo yalitolewa Oktoba 2024 lakini mpaka kufikia mwishoni mwa novemba kauli yake hiyo haijatekelezwa na msimu wa kilimo ndo huu, hakuna chochote kinachoendelea.

Wanakijiji walitii kwa kuorodhesha majina na kamati za ugawaji maeneo ziliundwa na vijiji lakini kimya kimekuwa kingi, hata kamati haijui kinachoendelea.

Maeneo yaliyotengwa hayajulikani mpaka kufikia novemba na mvua zimeanza kunyesha, Mkuu wa Wilaya naye hajasema lolote na msimu wa kuandaa mashamba na kulima umefika au alijua hakuna kitakachoendelea na kwamba alitoa maneno ya kisiasa?

Uamuzi uliochukuliwa na Wananchi ni kuendelea na kilimo katika mlima huo sababu ikiwa muda wa kilimo umefika na hawapewi majibu yoyote na wao wanaishi kwa kutegemea kilimo.
Screenshot_20241202-165710.png

Tetesi walizonazo maeneo wanayotaka kugaiwa tayari yana wamiliki, hawataki kuachia mkuu wa wilaya hajui anafanyaje naye anasubiri ngazi za juu na mashamba mapya ambayo ni msitu kwa sasa ni ngumu kwa mkulima mdogo kuziwahi mvua kwa sababu itabidi aanze kwa kukata miti kisha kulima.

Na kitu kingine wananchi wanadai hekari zilizotajwa na serikali kama fidia ni chache ukilinganisha na idadi ya wanaotakiwa kufidiwa. Hivyo hawako tayari kupewa hekari moja au mbili wakati mlimani walikuwa wanamiliki hekari nyingi na wengi wao waliuziwa na wazawa wa Kata hiyo.

Ushauri wangu kama kweli Serikali wanataka Wananchi waondoke katika mlima huo wapewe tu pesa kulingana na ukubwa wa eneo wakatafute wenyewe mashamba.

Screenshot_20241202-165448.png
 

Attachments

  • Screenshot_20241202-165435.png
    Screenshot_20241202-165435.png
    1.1 MB · Views: 5
  • Screenshot_20241202-165435.png
    Screenshot_20241202-165435.png
    1.1 MB · Views: 10
  • Screenshot_20241202-165448.png
    Screenshot_20241202-165448.png
    784.1 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241202-165448.png
    Screenshot_20241202-165448.png
    784.1 KB · Views: 5
Back
Top Bottom