Ruvuma: Watu 13 Matatani kwa kumzika mzee akiwa hai

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu 13 kwa tuhuma za kumzika, akiwa hai, Mzee Frolence Komba (78) katika makaburi ya shamba la Mungu yaliyopo Kijiji cha Mahanje, Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.

Chanzo ni tuhuma za kumhusisha mzee huyo kumuua mtoto wake Severine Komba (34) kwa imani za kishirikina.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Songea, baadhi wanafamilia ikiwemo watoto wa mzee huyo wamehusika pia kwenye tukio hili la kusikitisha.

Chanzo: ITV
 
Afrika haiendelei sababu ya[emoji116]
Wivu
Unafiki
Imani za kishenzi
Ushirikina
Acha wamzike tu kama kweli huyo mzee alikuwa mshirikina alitakiwa kufukiwa shimo kimo cha kisima ama atupwe kwenye mto wenye mamba afie huko, sio ajabu hawa washirikina ni waaribifu sana wa maisha ya watu, serikali ingekuwa inaamini hizi mambo basi ingefungua mahabusu kwaajili ya hawa walozi
 
Unamjuaje mshirikina?
 
Aaaagh, kwahiyo walimfunga kamba au, mi nasemaga, imani ndio ugonjwa mbaya kabisa wa akili kuwahi kuikumba hii dunia. Ni lini mtaanza kunielewa?! Si Uislam , si Ukrosto, si takataka nyingine yeyote, ni mental illness hiyo
Watakuelewa wachache mkuu.
Kuna watu wamekuwa watumwa kwa imani za kipumbavu wanashindwa kuchanganua mambo huku wamepewa kichwa naakili
 
Haupo sahihi ktk kufikiri kwako sababu hakuna imaninya dini inayoruhusu hayo.Hao waliofanya hivyo hawana imani ya kweli
 
Aaaagh, kwahiyo walimfunga kamba au, mi nasemaga, imani ndio ugonjwa mbaya kabisa wa akili kuwahi kuikumba hii dunia. Ni lini mtaanza kunielewa?! Si Uislam , si Ukrosto, si takataka nyingine yeyote, ni mental illness hiyo
Hakuna imani ya dini inaruhusu hayo kufanyika.Waliofanya hayo hawana imani ya kweli .Imani zinahimiza msamaha na kuwaonya na kuwaombea watu tukiwarekebisha kwa upendo
 
😂unapewa na Mungu umri mrefu Miaka 78 kumbe wanao wanaona unachelewa kufa
 
Afrika haiendelei sababu ya[emoji116]
Wivu
Unafiki
Imani za kishenzi
Ushirikina
Acha wamzike tu kama kweli huyo mzee alikuwa mshirikina alitakiwa kufukiwa shimo kimo cha kisima ama atupwe kwenye mto wenye mamba afie huko, sio ajabu hawa washirikina ni waaribifu sana wa maisha ya watu, serikali ingekuwa inaamini hizi mambo basi ingefungua mahabusu kwaajili ya hawa walozi
Kuamini ushirikina pia ni tatizo
 
Back
Top Bottom