Ruvuma: Wazee wadai kunyimwa dawa Hospitali ya Wilaya

Ruvuma: Wazee wadai kunyimwa dawa Hospitali ya Wilaya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Umoja wa wazee Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma, umewasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Laban Thomas wakiwatuhumu wahudumu wa Hospitali ya Wilaya hiyo kwa kuwanyima dawa, licha ya kutengewa dirisha lao katika hospitali hiyo.

Mkuu wa Mkoa Laban Thomas ametoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Aziza Mangosongo kuhakikisha wazee wanapata huduma stahiki na pia watumishi wabadili lugha wanayotumia kwa wazee.

Naye, Katibu wa Hospitali hiyo, Shukuru Msimbe amedai kuwa wazee wengi wana magonjwa makubwa kuliko uwezo wa dawa uliopo hospitalini hapo.

Source: Azam TV
 
Wazee hao wapewe bima ya afya bure kama anavyopewa mwinyi na kikwete. Wote walikuwa na mchango kwa taifa.
 
Back
Top Bottom