Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Miaka 10 iliyopita tuliuziwa eneo na Kijiji ambapo kipindi hicho kilikuwa kinaitwa Kijiji cha Liganga, tulilitumia eneo hilo kwa ajili ya kufanya kilimo.
Baadaye Jimbo lilipona eneo hilo linaleta faida kwa aradhi kukubali kilimo, wakaongeza mipaka ambayo ilikuwepo ili waweze kulichukua na eneo letu hilo.
Suala hilo lilifika hadi Mahakamani, Hakimu aliyekuwepo awali aliwaambia waliokuwa wamechukua eneo letu na tupo nao kwenye kesi kuwa hawajatenda haki kwa kuwa wamezidisha eneo wanalosema ni la kwao.
Wananchi ambao tunadai haki zetu za kuchukuliwa maeneo yetu tupo zaidi ya 500 na kuna ekari 1000.
Sisi ni raia ambao tunajichangacha, hatuna uwezo wa kushindana nao.
Wito wetu ni kuwa tunaomba Waziri wa Ardhi aje atusaidie kwa kuwa hizo bikoni zilizowekwa sasa hivi siyo halali, zimewekwa kwa lengo la kuchukua ardhi yetu sisi Wananchi wanyonge.
Hawa watu sisi tunashindwa kupambana nao kwa kuwa wana nguvu ya fedha kuliko sisi.
Sisi ni Watanzania na tuna haki ya kuishi maeneo yoyote yale, nyaraka ambazo zinaonesha tuliuziwa na Serikali ya Mtaa tunazo lakini hata baadhi ya wale waliotuuzia nao wametugeuka kwa kuwa wanashirikiana na hao washindani wetu.
Waziri wa Ardhi akija pamoja na maafisa wake wa Wizara wakapima na kubaini kuwa kweli eneo tunalolipigania lipo ndani ya bikoni ambazo zilikuwepo awali, sisi tutaondoka kwa amani lakini pia ikibainika wao ndio wameingilia eneo letu na kutotenda haki basi watuache tuishi kwa amani.
Pamoja na hivyo tunamuomba Mbunge wetu Jenista Mhagama naye awepo katika timu hiyo, Wananchi wake tunateseka.
Nimeambatanisha baadhi ya nyaraka zinazoonesha tulinunua kwa halali kwa kufuata hatua za Kiserikali: