RUWASA Mnachelewesha Sana Malipo ya Wakandarasi

RUWASA Mnachelewesha Sana Malipo ya Wakandarasi

DISPLEI

Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
73
Reaction score
47
Kuna Kandarasi nyingi za miradi ya maji chini ya RUWASA zinazoendelea na zilizokamilika lakini malipo yanachelewa sana. Watendaji wa RUWASA kuanzia ngazi za wilaya hadi makao makuu hawaonekani kujali machungu wanayoyapata wakandarasi kutumia hela zao kutekeleza maradi hii. Kuna madeni ya mabenki na hela za moto kutoka kwa wakopeshaji binafsi, riba zinaongezeka kiasi cha wakandarasi kuuziwa mali zao. Pia hawa watu wanadaiwa na mafundi pamoja na wafanyakazi wengine hadi kutishiana amani. Inakuwaje mradi ukamilike mkandarasi anakaa ziadi ya miezi 3 hadi hata mwaka anafuatilia malipo hayatoki?

Kibaya miradi hii ambayo wakandarasi wanadai malipo kwa kipindi kirefu bado inatumika kunadi sera katika kapeni za uchaguzi zinazoendelea kuhusu utekelezaji wa Ilani 🙄🙄! . Wahusika kupitia jukwaa hili watambue kwamba wanachangia sana ugumu wa maisha ambao ndo kilio cha wananchi hela unaingiza kwenye mradi halafu hulipwi unaanza kuangaika kukimbizana na mabenki pamoja na wakopeshaji na bado madai ya mafundi na wafanyakazi wengine waliotekeleza mradi. Wahusike tuweni na huruma kandarasi zilipwe kwa wakati ili maisha yaendelee, inaumiza saana.

RUWASA pamoja na taasisi zingine zinazodaiwa, fanyeni kitu malipo kukaa zaidi ya siku 30 inaumiza sana na inaongeza umaskini kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom