Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
Karibu jamvini na asante kwa mawazo constructive.Hodi hodi wana bodi! Naomba mnipokee ndiyo mara yangu ya kwanza nachangia.
Ibra Mo, pamoja na yote ulioyasema ambayo na mazuri ya kufanyiwa kazi na Chadema, pia waanze kuanzia sasa kuwa na orodha yote ya vituo vilivyopigia kura mwaka huu ili iwasadie kuwa na idadi ya mawakala wa 2015 watayarishe bajeti kuanzia sasa. Itakpofika hiyo 2015 watakuwa wamejiweka mahali pazuri kwa kushindana bila ya kuwa na wasiwasi wa fedha ya kuwalipa wakala.Mimi naliona hili lilkuwa ni tatizo kwa vyama vingi VYA UPINZANI. Haya ni maoni yangu.
Viongozi wote wa juu wa Chadema ni membazi hapa dugu yangu. Hakuna wasiloliona.Sawa kabisa, hivi hawa vionguzi wanapita pita humu?
DC
Ni kweli ruzuku peke yake haitoshi lakini kupanga ni kuchagua, hakuna siku mtu atasema hela imetosha hela huwa haijai mfukoni, ila ukitaka zijae zipangilie uwe na priorities. CCM wao matumizi yao yanajulikana tunajua zinapoishia ndiyo maana leo tunawashauri Chadema wasifanye hayo madudu. Niliwahi kusikia choo kimoja chenye matundu sijui matano kinajengwa kwa Mil. 700(ni mfano tu), kama matunizi yenyewe ndiyo ya aina hiyo hata upewe ruzuku ya bil.10 kwa mwezi haziwezi kutosha.
Kwa ufupi michango ya wanachadema walio na uchungu wa nchi kuona inaleta mbadiliko ya kweli ni ya muhimu sana saaaaaaaaaana na ruzuku ambayo nadhani itasaidia kidogo kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya nchi nzima, hivyo naamini tunahitaji michango mingi kuliko kufikiria ruzuku tu. tutafika tuendako.
Hima viongozi wekeni mikakati kuanzia sasa. Nawaaminia sana viongozi wa Chadema kwa mikakati. Ninatumaini sana nao.
Asante sana DC kwa mawazo constructive,Kwenye suala la ruzuku tuko pamoja. Ila mimi nilitaka kupanua mjadala kwa kuingiza hoja ya kukichangia chama kama njia muhimu ya kukisogeza zaidi kwa wananchi. Kama watu watakuwa makini basi watatambua kuwa ruzungu ni bait inayotumiwa na CCM kuviua vyama. Kwa sababu viongozi wengi wanaokuwa upinzani wanakuwa wamepigika sana, kwa hiyo ikimwagika ruzuku ya kutosha wote wanaikodolea macho na kusababisha vita isiyo na mwamuzi. CHADEMA wamewenza kujenga chama bila ruzuku ya maana kwa hiyo inabidi waukwepe sana huo mtego wa ruzuku.
Hilo ndilo lililomaanisha..you pay for something then you own it...and thus you can value and protect it against any evils. Hiyo ndiyo filosofia ambayo viongozi wa CHADEMA wanatakiwa kuipa kipaumbele. Ilisaidia sana enzi za TANU na kwa hiyo CHADEMA kwa sasa iko kwenye nafasi nzuri ya kuitumia nguvu ya umma kuchagiza mabadiliko zaidi. It's very possible!
Asante sana DC kwa mawazo constructive,
Ni jukumu la viongozi wa Chadema kutembelea humu na kuchukua mawazo ya aina hii kwa sababu tunaoyatoa ni watanzania hao hao wapiga kura wao, kwa vile si wote wenye uwezo wa kufika ofisini na kuzungumza.