Elections 2010 Ruzuku ya Chadema

Elections 2010 Ruzuku ya Chadema

Hodi hodi wana bodi! Naomba mnipokee ndiyo mara yangu ya kwanza nachangia.
Ibra Mo, pamoja na yote ulioyasema ambayo na mazuri ya kufanyiwa kazi na Chadema, pia waanze kuanzia sasa kuwa na orodha yote ya vituo vilivyopigia kura mwaka huu ili iwasadie kuwa na idadi ya mawakala wa 2015 watayarishe bajeti kuanzia sasa. Itakpofika hiyo 2015 watakuwa wamejiweka mahali pazuri kwa kushindana bila ya kuwa na wasiwasi wa fedha ya kuwalipa wakala.Mimi naliona hili lilkuwa ni tatizo kwa vyama vingi VYA UPINZANI. Haya ni maoni yangu.
Karibu jamvini na asante kwa mawazo constructive.
 
Kwa ufupi michango ya wanachadema walio na uchungu wa nchi kuona inaleta mbadiliko ya kweli ni ya muhimu sana saaaaaaaaaana na ruzuku ambayo nadhani itasaidia kidogo kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya nchi nzima, hivyo naamini tunahitaji michango mingi kuliko kufikiria ruzuku tu. tutafika tuendako.
Hima viongozi wekeni mikakati kuanzia sasa. Nawaaminia sana viongozi wa Chadema kwa mikakati. Ninatumaini sana nao.
 
Luteni nakubaliana nawe ingawaje ununuzi wa magari si lazima sana tunaweza kuanza hata na pikipiki.
Kitu ambacho tuelewe tunaotaka kuona mabadiliko kama alivosema Park City inatakiwa tuwe tayari kuchangia chama. Pesa za ruzuku hazitoshi na lazima tuwe tayari kuchangia chama kinachoonekana cha nguvu kama CHADEMA.
Tunachoomba viongozi wa CHADEMA wawe makini vitu vifuatavo:
1. Imani kwa wananchi. Mnapigania ufisadi na wananchi tunawaonga mkono mkichezea imani yetu kwenu na kuanza ubadhirifu kwenye ruzuku na michango ya wananchi mtaporomoka vibaya.
2. Njama za kuigawa chama. Migogoro na malalamiko ndani ya chama isiachwe bila kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu na wa kisayansi. CCM watatafuta mbinu za kuwafarakanisha kwa mbinu chafu kama udini na ukabila.
3. Wajenge sura ya kitaifa hasa kwenye uongozi. CHADEMA inapendwa na wasomi na hivo ina nafasi ya kuondoa dhana zinazojengwa juu yake kwa kuunda uongozi wenye sura ya kitaifa kwa kutumia hao wasomi. Ni muhimu kuwa makini sana hapa kwa kuhakikisha wanapatikana watu wa kujitolea na viongozi hasa. Sisemi kuwa Mbowe au Dr. Slaa waondoke kwenye uongozi ila kuna haja ya kufuta dhana ya ukaskazini kwenye chama.
3. Mpiganie tume huru ya uchaguzi kwa gharama yoyote.
 
DC

Ni kweli ruzuku peke yake haitoshi lakini kupanga ni kuchagua, hakuna siku mtu atasema hela imetosha hela huwa haijai mfukoni, ila ukitaka zijae zipangilie uwe na priorities. CCM wao matumizi yao yanajulikana tunajua zinapoishia ndiyo maana leo tunawashauri Chadema wasifanye hayo madudu. Niliwahi kusikia choo kimoja chenye matundu sijui matano kinajengwa kwa Mil. 700(ni mfano tu), kama matunizi yenyewe ndiyo ya aina hiyo hata upewe ruzuku ya bil.10 kwa mwezi haziwezi kutosha.

Kwenye suala la ruzuku tuko pamoja. Ila mimi nilitaka kupanua mjadala kwa kuingiza hoja ya kukichangia chama kama njia muhimu ya kukisogeza zaidi kwa wananchi. Kama watu watakuwa makini basi watatambua kuwa ruzungu ni bait inayotumiwa na CCM kuviua vyama. Kwa sababu viongozi wengi wanaokuwa upinzani wanakuwa wamepigika sana, kwa hiyo ikimwagika ruzuku ya kutosha wote wanaikodolea macho na kusababisha vita isiyo na mwamuzi. CHADEMA wamewenza kujenga chama bila ruzuku ya maana kwa hiyo inabidi waukwepe sana huo mtego wa ruzuku.

Kwa ufupi michango ya wanachadema walio na uchungu wa nchi kuona inaleta mbadiliko ya kweli ni ya muhimu sana saaaaaaaaaana na ruzuku ambayo nadhani itasaidia kidogo kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya nchi nzima, hivyo naamini tunahitaji michango mingi kuliko kufikiria ruzuku tu. tutafika tuendako.
Hima viongozi wekeni mikakati kuanzia sasa. Nawaaminia sana viongozi wa Chadema kwa mikakati. Ninatumaini sana nao.

Hilo ndilo lililomaanisha..you pay for something then you own it...and thus you can value and protect it against any evils. Hiyo ndiyo filosofia ambayo viongozi wa CHADEMA wanatakiwa kuipa kipaumbele. Ilisaidia sana enzi za TANU na kwa hiyo CHADEMA kwa sasa iko kwenye nafasi nzuri ya kuitumia nguvu ya umma kuchagiza mabadiliko zaidi. It's very possible!
 
Kwenye suala la ruzuku tuko pamoja. Ila mimi nilitaka kupanua mjadala kwa kuingiza hoja ya kukichangia chama kama njia muhimu ya kukisogeza zaidi kwa wananchi. Kama watu watakuwa makini basi watatambua kuwa ruzungu ni bait inayotumiwa na CCM kuviua vyama. Kwa sababu viongozi wengi wanaokuwa upinzani wanakuwa wamepigika sana, kwa hiyo ikimwagika ruzuku ya kutosha wote wanaikodolea macho na kusababisha vita isiyo na mwamuzi. CHADEMA wamewenza kujenga chama bila ruzuku ya maana kwa hiyo inabidi waukwepe sana huo mtego wa ruzuku.

Hilo ndilo lililomaanisha..you pay for something then you own it...and thus you can value and protect it against any evils. Hiyo ndiyo filosofia ambayo viongozi wa CHADEMA wanatakiwa kuipa kipaumbele. Ilisaidia sana enzi za TANU na kwa hiyo CHADEMA kwa sasa iko kwenye nafasi nzuri ya kuitumia nguvu ya umma kuchagiza mabadiliko zaidi. It's very possible!
Asante sana DC kwa mawazo constructive,

Ni jukumu la viongozi wa Chadema kutembelea humu na kuchukua mawazo ya aina hii kwa sababu tunaoyatoa ni watanzania hao hao wapiga kura wao, kwa vile si wote wenye uwezo wa kufika ofisini na kuzungumza.
 
nakubaliana nawe mkuu,safi sana naamini watakuwa wameidaka hii
 
Asante sana DC kwa mawazo constructive,

Ni jukumu la viongozi wa Chadema kutembelea humu na kuchukua mawazo ya aina hii kwa sababu tunaoyatoa ni watanzania hao hao wapiga kura wao, kwa vile si wote wenye uwezo wa kufika ofisini na kuzungumza.

Ni kweli ila pia wengine tunatakiwa kujitolea. Kama unaweza kupata nafasi si vibaya kupiga simu ukaongea na kiongozi wa CHADEMA ili mradi unatafuta yule msikivu atakaye kusikiliza. Njia nyingine ni kuwaandikia kile ambacho wewe binafsi ungepenza kuona kinafanyiwa kazi. Na kama maoni yanayotolewa hapa, unaweza pia kuyaunganisha vizuri na kuwatumia. Inabidi Watanzania tubadilike na tuwe tayari kulipa gharama ya mabadiliko. Tukiwaachia wachache wailipe hata yakishapatikana hao wachache wataanza kutafuta faida kwanza na tutakuwa tumeruka mkoja na kukanyaga kimba chenyewe! That will be a pity!
 
Viongozi wote wa Chadema nikimaanisha top leadership ni wanachama hapa na huwa wanasoma michango hii. Nina imani they are reading these ideas.
 
Back
Top Bottom