#COVID19 Rwanda imetumia jiwe moja kuua ndege watatu kwa pamoja

#COVID19 Rwanda imetumia jiwe moja kuua ndege watatu kwa pamoja

Yussufhaji

Member
Joined
Sep 9, 2018
Posts
35
Reaction score
28
30/11/2021

Hatua hii ya Rwanda kuweka marufuku ya usafiri dhidi ya Afrika Kusini kwa kisingizio cha aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 kinachojulikana kama "Omicron" ambacho kimegunduliwa nchini Afrika Kusini haishangazi,

Rwanda inajua inachokifanya, inawezekana sababu ya awali ikawa ni kulinda raia wake, bali pia marufuki hii inakwenda mbali zaidi hata kulinda uchumi wake,

Wakati gwiji wa soka duniani Lionel Messi akiihama Klabu yake ya Bercelona na kufanya usajili PSG alionekana akiwa na jenzi yenye maandishi nyuma"Visit Rwanda"

Naam, Rwanda imewekeza vya kutosha katika kuutangaza utalii wake, imewahi pia kushirikiana na klabu ya Arsenal ya Uengereza kuutangaza utalii wa nchi hiyo, hivyo marufuku hii inajibebea pointi muhimu kama miongoni mwa sehemu salama kwa utalii na uwekezaji barani Afrika,

Hatua hii walio ichukua inakwenda kulinda sekta ya utalii nchini Rwanda na uchumi kwa ujumla,

Lakini pia, mbali ya kulinda Uchumi na Wananchi wake, inawezekana pia Rwanda ikawa inalinda maslahi yake ya kisiasa,

Unaweza kusema Rais Kagame anajaribu kutunisha msuli wake, waswahili wanasema Adui usiemuweza umvizie wakati muafaka umtandike,

Mwaka 2014 nchi hizi mbili ziliingia katika mgogoro wa kidiplomasia baada ya aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Rwanda kufariki katika hali ya kustaajabisha katika moja ya hoteli Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, ambapo ilisemekana serikali ya Rwanda ilihusika na kifo hicho baada ya Kanali Patrick Karegeya kugeuka mwiba kwa serikali ya Kigali,

Muda mwingi huwa ninashauri tusiogope kutumia mbinu za Kibepari kufanikisha au kulinda maslahi yetu, hicho ndicho wanachokifanya Rwanda wakati huku.

Na
Yussuf H. Khatib
Mtoto wa Mkulima

Email: hajjyussuf2@gmail.com
WhatsApp: wa.me/+255777158131
fb: Kirjaudu sisään Facebookiin

IMG_20211130_144034.jpg
FB_IMG_16382717456373177.jpg
FB_IMG_16382118774995169.jpg
 
Back
Top Bottom