Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Waziri wa Afya wa Rwanda Daniel Ngamije amesema wizara yake imepanga kusambaza roboti kwenye vituo vya kutibu virusi vya Corona na maeneo mengine ya umma.
Akiongea kupitia televisheni waziri Ngamije amesema Roboti tano zilizoagizwa kutoka nje ambazo zimepewa majina ya Kinyarwanda zitatumika kama kiunganishi kati ya dokta na mgonjwa, na hivyo kupunguza mawasiliano ya binadamu na hatari za kusambaa kwa virusi.
Waziri Ngamije amesema mbali na kutumika kwenye vituo vya matibabu, roboti hizo pia zitatumika kupima joto kwenye maeneo ya umma kama vile vituo vya mabasi na milango ya kuingilia maduka ya manunuzi, na kwamba baadhi ya roboti tayari zimeshafika Rwanda ambapo zitawekewa programu na kusambazwa kwanza.
Kwa mujibu wa wizara ya afya ya nchi hiyo hadi kufikia Ijumaa jioni, Rwanda imethibitisha wagonjwa wa virusi vya Corona 273, wakiwemo waliopona 136.