Rwanda na DRC mbabe anajulikana, busara zitumike

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
WanaJf, Hi!
Nchi ya Rwanda na DRC ni majirani zetu kabisa na ni washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata hivyo matukio ya usimikaji na ufadhili wa kundi la M23 unaofanywa na nchi ya Rwanda hatuwezi kuubariki katu sababu madhara kwa raia ni MENGI sana.

Sasa hata iwe vipi iwapo nchi hizi zitaamua kumaliza mgogoro huu kwa mtutu wa bunduki mbabe anajulukana "Ni nchi ya DRC". Kwa kuwa kitakwimu nchi hii ina idadi ya watu 92,000,000 huku Rwanda ikiwa na watu 13,000,000. Hivyo, DRC inaizidi Rwanda takribani watu 79,000,000. So technically DRC anahitaji kitu kidogo sana kushinda vita hiyo nacho ni raslimali fedha za kumudu kazi.

Rwanda asipotumia busara atajilaumu kwa hii vita anayoenda kuanzisha. Nchi wanachama wa EA (Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, na Sudan) waingilie kati haraka. Madhara yajayo ni makubwa ingawa binafsi PK simpendi kabisa.

Heri nusu shari kuliko shari kamili.

Msakila M Kabende
Jf Member
 
mbabe anajulukana "Ni nchi ya DRC". Kwa kuwa kitakwimu nchi hii ina idadi ya watu 92,000,000 huku Rwanda ikiwa na watu 13,000,000.
Hoja uduvi hii. Ubabe wa nchi haupimwi kwa idadi ya watu, bali unapimwa kwa weledi wa jeshi. Rwanda Ina jeshi lenye weledi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki.

Ndiyo maana Israeli ni taifa dogo Sana lkn linapokuja suala la we lwdi wa jeshi wanaongoza
 
KUna mahala nilisoma kuwa PK anatumika na wakubwa no wonder ana iyo jeuri.
Lakini pia wakuu wengi wa jeshi la DRC Ni watutsi apo inafnay vita iwe ngumu ina inaweza pelekea kusalitiana mbele ya safari.
Ila this has been dragging for long naona wazichape tuu maana naona M23 wanaendelea kuchukua maeneo ya DRC na kama raisi huwezi kaa kimya ni kichapo kwanza.
Baada ya kichapoo nadhani heshima itakuja tuu
 
Sasa hata iwe vipi iwapo nchi hizi zitaamua kumaliza mgogoro huu kwa mtutu wa bunduki mbabe anajulukana "Ni nchi ya DRC". Kwa kuwa kitakwimu nchi hii ina idadi ya watu 92,000,000 huku Rwanda ikiwa na watu 13,000,000. Hivyo, DRC inaizidi Rwanda takribani watu 79,000,000. So technically DRC anahitaji kitu kidogo sana kushinda vita hiyo nacho ni raslimali fedha za kumudu kazi.
Mkuu 'Kabende Msakila'

Kuna funzo kubwa sana hapa ambalo wengi wanashindwa kulipa umuhimu wake; kwamba uwingi au ukubwa wa nchi si hoja, bali kitu muhimu zaidi ya yote katika nchi yoyote ile ni jinsi watu wake wanavyojitambua na kuelewa maana ya umoja wao kuwa nchi.

Katika hali ya kawaida, DRC siyo taifa la kuchezewa na hivi vi nchi kama Rwanda au Uganda, lakini angalia wanavyohangaishwa sasa, kama watoto wadogo.

Kwa hiyo, kwa kifupi tu, ni kwamba DRC inatakiwa kuacha hii tabia ya kulialia, huku ikilizwa na vinchi visivyokuwa na chochote ila kujivimbisha tu vionekane navyo vimo.
DRC ijipange na iamue yenyewe kwamba sasa inataka kutambulika kama taifa lisiloweza kuchezewa na yeyote katika ukanda huu na hata nje ya Afrika.

Viongozi wa Kongo wakiamua na kuwaongoza na kuwapanga wananchi wao na jeshi lao, haiwezi kuchukua zaidi ya mwezi mmoja kusafisha kabisa vikundi vinavyoihangaisha sasa hivi nchi hiyo kwa kutumiwa na hivi vinchi jirani.
 
Hoja uduvi hii. Ubabe wa nchi haupimwi kwa idadi ya watu, bali unapimwa kwa weledi wa jeshi. Rwanda Ina jeshi lenye weledi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki.

Ndiyo maana Israeli ni taifa dogo Sana lkn linapokuja suala la we lwdi wa jeshi wanaongoza
Hata ya kwako hii siyo hoja, bali ni "hoja Minyoo".

Rwanda hana kitu. Kujivimbisha hakuifanyi iwe na "jeshi lenye weledi" kama unavyohadaika wewe.

Hivi "weledi" una hati miliki?
 
Rwanda huwa siwaamini kama walichinjana kama kuku back in the days. Watapigwa ka nchi kenyewe kama Kibaigwa.
 
Hoja uduvi hii. Ubabe wa nchi haupimwi kwa idadi ya watu, bali unapimwa kwa weledi wa jeshi. Rwanda Ina jeshi lenye weledi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki.

Ndiyo maana Israeli ni taifa dogo Sana lkn linapokuja suala la we lwdi wa jeshi wanaongoza
Israel wanaongoza kwa teknolojia si uwezo wa vita ya mguu - Rwanda ni dhaifu sana kwa DRC
 
Rais wa DRC,akazie hapo hapo,kama ni vita iwe vita tu,kwani sasa naona dunia nzima imeshituka kuliko kila siu mazungumzo tu bila mafanikio,sasa kuanzia EAC,AU,UN na EU,wameanza kuona sasa kinachoenda kutokea sio kitu kizuri!!bahati nzuri na wananchi wake karibu wote wako nyuma yake.
 
Israel wanaongoza kwa teknolojia si uwezo wa vita ya mguu - Rwanda ni dhaifu sana kwa DRC
Wewe ni hater wa Kagame na unachoandika ni ushabiki zaidi, inajulikana Congo kila mkitembezewa kichapo na M23 mnamsingizia Kagame, Rwanda hawana wanajeshi Congo wanaopigana na wacongo, wanaopigana na serikali ni factions nyingi tuu ndani ya Congo na mojawapo ni M23 ambao nao ni wacongo , Rwanda hawana shida na Congo zaidi ya FDLR, kaeni chini na hizo factions mpate amani au wachapeni mshinde vita sio kila siku kulia lia tuu kama panya
 
Tatizo DRC haina jeshi bali ni walinzi wa KKbsecurity
 
WanaJf, Hi!
Nchi ya Rwanda na DRC ni majirani zetu kabisa na ni washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata hivyo matukio ya usimikaji na ufadhili wa kundi la M23 unaofanywa na nchi ya Rwanda hatuwezi kuubariki katu sababu madhara kwa raia ni MENGI sana.

Sasa hata iwe vipi iwapo nchi hizi zitaamua kumaliza mgogoro huu kwa mtutu wa bunduki mbabe anajulukana "Ni nchi ya DRC". Kwa kuwa kitakwimu nchi hii ina idadi ya watu 92,000,000 huku Rwanda ikiwa na watu 13,000,000. Hivyo, DRC inaizidi Rwanda takribani watu 79,000,000. So technically DRC anahitaji kitu kidogo sana kushinda vita hiyo nacho ni raslimali fedha za kumudu kazi.

Rwanda asipotumia busara atajilaumu kwa hii vita anayoenda kuanzisha. Nchi wanachama wa EA (Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, na Sudan) waingilie kati haraka. Madhara yajayo ni makubwa ingawa binafsi PK simpendi kabisa.

Heri nusu shari kuliko shari kamili.

Msakila M Kabende
Jf Member
Mwaka 1967, Israeli ilizishinda nchi za Misri, Algeria, Iraq, Morocco, Jordan, Syria, Lebanon, Saudi Arabia na nyingine zote za kiarabu. Israeli ni nchi ndogo sana na idadi ya watu pia ni ndogo. Kwaiyo ukubwa wa nchi na idadi ya watu siyo kigezo pekee cha kushinda vita. Kuna kitu zaidi ya hapo
 
Hoja mfu
Israel wapo mil 9, Nigeria wapo mil 200. Unataka kusema Nigeria inaweza kushinda Vita dhidi ya Israel?
 
Jeshi la DRC ni maarufu kwa kunywa pombe na kubaka Wanawake wa Kikongo.

Watapigana saa ngapi, ni Jeshi lisilo na nidhamu kuliko yote Barani Afrika.

Utamsaidia mtu ambae akiwaona tu M23 anatupa silaha na kuvaa nguo za Kiraia na kukimbia, jioni unamkuta Bar anawapiga kwala apewe Bia za bure.
 
kila mkitembezewa kichapo na M23 mnamsingizia Kagame, Rwanda hawana wanajeshi Congo wanaopigana na wacongo, wanaopigana na serikali ni factions nyingi tuu ndani ya Congo na mojawapo ni M23 ambao nao ni wacongo , Rwanda hawana shida na Congo
Pole, hujui ulinenalo.
 
Rwanda hawana shida na Congo zaidi ya FDLR
Wanyarwanda walishasema "NEVER AGAIN MAUAJI YA KIMBARI"

Na sisi Tanzania hatuwezi kukaa na kuangalia Mauwaji mengine ya Kimbari

FLDR waweke silaha chini warudi Rwanda.
 
WanaJf, Hi!
Nchi ya Rwanda na DRC ni majirani zetu kabisa na ni washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata hivyo matukio ya usimikaji na ufadhili wa kundi la M23 unaofanywa na nchi ya Rwanda hatuwezi kuubariki katu sababu madhara kwa raia ni MENGI sana.

Sasa hata iwe vipi iwapo nchi hizi zitaamua kumaliza mgogoro huu kwa mtutu wa bunduki mbabe anajulukana "Ni nchi ya DRC". Kwa kuwa kitakwimu nchi hii ina idadi ya watu 92,000,000 huku Rwanda ikiwa na watu 13,000,000. Hivyo, DRC inaizidi Rwanda takribani watu 79,000,000. So technically DRC anahitaji kitu kidogo sana kushinda vita hiyo nacho ni raslimali fedha za kumudu kazi.

Rwanda asipotumia busara atajilaumu kwa hii vita anayoenda kuanzisha. Nchi wanachama wa EA (Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, na Sudan) waingilie kati haraka. Madhara yajayo ni makubwa ingawa binafsi PK simpendi kabisa.

Heri nusu shari kuliko shari kamili.

Msakila M Kabende
Jf Member
Uelewa wako kuhusu mambo ya vita ni mdogo sana, umeshawahi kujiuliza nchi zote za Kiarabu zinashindwa vipi kuikabili Israel [emoji1134]?
 
Hoja uduvi hii. Ubabe wa nchi haupimwi kwa idadi ya watu, bali unapimwa kwa weledi wa jeshi. Rwanda Ina jeshi lenye weledi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki.

Ndiyo maana Israeli ni taifa dogo Sana lkn linapokuja suala la we lwdi wa jeshi wanaongoza
Hoja dhaifu zaidi, ili DRC itulie yupo kiongozi anatakiwa aondoshwe.
 
Uelewa wako kuhusu mambo ya vita ni mdogo sana, umeshawahi kujiuliza nchi zote za Kiarabu zinashindwa vipi kuikabili Israel [emoji1134]?
Israel ipo saported na US, UK, GERMAN NA MATAIFA MAKUBWA YOTE na si Rwanda. DRC akikomaa wananyooka mchana peupe
 
Back
Top Bottom