Raphael Thedomiri
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 442
- 729
Wataalam huru wa Umoja wa Mataifa wamesema jeshi la Rwanda lilihusika kwenye ‘operesheni za kijeshi‘ dhidi ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo yanayokumbwa na machafuko mashariki mwa Congo.
Kulingana na ripoti ya wataalam hao ambayo shirika la habari la AFP limepata nakala yake, kuna ushahidi wa kutosha kwamba jeshi la Rwanda liliingilia kati moja kwa moja katika vita vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya waasi wa kundi la M23, na kwamba jeshi hilo liliwaunga mkono waasi hao kwa kuwapa silaha, risasi na magwanda au sare za kivita.
Ripoti hiyo inajiri mnamo wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuliunga mkono kundi la M23.
Msemaji wa serikali mjini Kigali alikanusha madai kwamba Rwanda iliwaunga mkono waasi wa M23. Aidha alikataa kuzungumzia tuhuma nyinginezo dhidi ya Rwanda hadi pale ripoti hiyo ilipochapishwa rasmi.
Chanzo dw