Rwanda Yaandika Historia! Kagame Afanikiwa Kuileta Formula 1 Afrika!

Rwanda Yaandika Historia! Kagame Afanikiwa Kuileta Formula 1 Afrika!

Ila kuna watu hua hata hawaeleweki wanataka nini,

Hapa utakuta kuna mtu anaisifu Rwanda kwa kuandaa F1 ila siku nchi yake nayo ikitaka kuandaa,atakuja kulalamika hapa,F1 ya nini wakati hatuna madawati,Barabara mbovu,hatuna madawa...
Nchi inaandaa AFCON, kuna watu wanataka kukiwasha kipindi cha Afcon; halafu wanamsifia PK na F1 Huku wanasema ni dikteta. Ngumu sana kuelewa
 
Tunaweza muita Kagame dikteta, lakini mwamba ana maono ya mbali kwa nchi yake. Wakati sisi tunaishia kusema Arusha itakuwa Dubai ya Afrika, yeye anachukua hatua. Tusishangae miaka 20 ijayo Rwanda ndo ikawa Dubai ya Afrika
Angeendekeza domokrasia ya chagadomoz na chale heche Rwanda ingekuana Burundi
 
kitu ambacho sijaelewa mpaka leo khs rwanda, wanafanya mambo makubwa sana wkt mwingine unafikiri kwamba wako over ambitious lkn gdp per capital ya rwanda bado ni ndogo sana tena sana tu ni kama 1,290 usd vs tanzagiza 1,280 usd (kwa mujibu wa wikipedia) lkn ukisikia mambo ambayo wanafanya unashangaa i mean, wana-sponsor aston villa football club ya england ambapo rwanda ana-transfer 20 million usd kila mwaka to england (kila mwaka wanapeleka >50 billion tanzanian shillings to england kulipia mipira), wameleta tour de rwanda ambayo ni kama tour de france yale mashindano ya baiskeli maarufu duniani ya ufaransa, mara sijui flying taxes, na mnasema wanaleta f1 formula one, sasa kwa nini hai-translate into economic growth kwa wanyarwanda au hainekani kwenye gdp at least? kwa maana pato la mnyarwanda bado ni dogo sana, bado ni one of the poorest people on earth hawajafikia hata tu lower middle income status tuliyofikia kabla ya kuondolewa baada ya hii regime kuja.

hivyo sielewi hii hype yote ya rwanda ni ya nini kama haisadii wananchi chochote? i mean, hosting f1 siyo jambo dogo unahitaji wananchi pia waweze kumudu kununua tiketi na mambo mengine mengi sasa kama wananchi ni one of the poorest in world hamuoni kwamba wanatupa tu fedha?

na ndiyo maana democracy ni muhimu kwani kama wangekuwa na multiparty democarcy upinzani wangehoji na kuwashitaki kwa wananchi lkn ni one man show anachoamua raisi kinafanyika inaweza kuwa sawa kama mkibahatika kuwa na kiongozi ambaye kweli anaweka maslahi ya watu wake kwanza na siyo binafsi lkn ni mara chache sana inatokea hivyo wengi wao kwenye udikteta its abojut stealing and stealing na kwa kuwa wanaiba ni lzm wajilinde na wanaweza tu kujilinda wakiwa na power hivyo inakuwa ni vicious circle ...
 
Hapa inakuwa discussed Rwanda; ukiweka kiujumla jumla unakuwa hueleweki kwa msomaji wako; na mimi nkauliza maswali mawili mepesi kabisa
Nime compare region yetu na nchi zingine nikaja na nilico andika
 
Zitaje hizo Nchi
Sasa unajiita smart dude halafu hujui silicon valley inakopatikana na how much the country and taxpayers benefit from it?

Nikikuleta kwenye swala la indirect benefits anazo pata USA kutokana na dollar inayotumika sana duniani
Kupitia mambo kama exorbitant privilege na seigniorage tutaelewana kweli?
 
Sasa unajiita smart dude halafu hujui silicon valley inakopatikana na how much the country and taxpayers benefit from it?

Nikikuleta kwenye swala la indirect benefits anazo pata USA kutokana na dollar inayotumika sana duniani
Kupitia mambo kama exorbitant privilege na seigniorage tutaelewana kweli?
Umejikamua mpaka umebold…. Angalia usije ukatoa kimba kabisa
 
Huu ni mchezo mmojawapo ulionipita kando kama baseball, boxing na cricket. Nikiangalia magari yanavyogongana wakati mwingine yanawaka moto, hapana!!!!
Technology imekua mzee! Hayo magari yanacollide yanamong'onyoka na dereva anatoka mzima kabisa! Zamani ajali ziliwaua sana madereva!
 
Sasa unajiita smart dude halafu hujui silicon valley inakopatikana na how much the country and taxpayers benefit from it?

Nikikuleta kwenye swala la indirect benefits anazo pata USA kutokana na dollar inayotumika sana duniani
Kupitia mambo kama exorbitant privilege na seigniorage tutaelewana kweli?
Kwamba unafanya conparison ya USA na hizi nchi zetu? Hii peke yake ni fallacy. Halafu kwenye uzi wa Rwanda? Haya Mkuu, all the best
 
Samia anapambana kufanya hayo ila ndio vita kubwa sana anakabiliana nayo
Kapata CHAN na Sasa AFCON si mashindano madogo ila na huko angefika kama angepata support
 
Kubwa sana.... Yaani kwa ukubwa wake ni kwamba hata Tanzania itaenda kufaidika hasa kwenye sekta ya utalii... F1 huwa inakusanya matajiri na celebrities wa kutosha na ninaamini wengi hawataondoka East Africa bila kutembelea baadhi ya vivutio vyetu vikubwa kama Serengeti au kwenda kupumzika Zanzibar

Tena, ikifika wakati huo, kama hazipo, basi ziwepo at least temporary direct flights from Arusha/Zanzibar to Rwanda and back
yeah sahihi
 
Back
Top Bottom