Rwanda yafunga makanisa 4,000 na misikiti 100 iliyokiuka vigezo vya usalama

Rwanda yafunga makanisa 4,000 na misikiti 100 iliyokiuka vigezo vya usalama

Rwanda imefunga maelfu ya makanisa na misikiti katika kile serikali ya nchi hiyo inachosema ni kushindwa kukidhi vigezo vya usalama na afya.

Je, Kuna miongozo yoyote ya usalama na afya kwa makanisa na misikiti Tanzania? Tunahitaji kumuiga Kagame katika hili, amefanikwa sana kuiweka nchi ya Rwanda katika mstari ulionyooka kuhusiana na masuala ya kidini.

20240809_163447.jpg

 
Kuna miongozo yoyote Tanzania ya idadi ya watu na mitungi ya zimamoto makanisani na misikitini??
 
Katika hili, namuunga mkono dikteta PK.

Na Tanzania nayo ipige marufuku kufungwa vipaza sauti juu ya nyumba za ibada, na hivyo kuwasababishia watu kelele. Iwe ni marufuku kufungulia mziki kwa sauti ya juu nyakati za usiku kwenye nyumba za ibada.
Wachungaji, manabii, mitume, na maaskofu wote lazima wawe na elimu ya teolojia.

Iwe ni marufuku kwa manabii/mitume kuwahadaa watu eti wanaponya ukimwi, kisukari, kansa, wanafanya miujiza ya kupata utajiri, nk. Huu ni utapeli wa wazi kabisa.
 
Kagame anakosea aache maandiko yatimie tuachane na hii dunia ya wanyang'anyi...yeye sio Mungu aweze kutambua makanisa mazuri na mabaya
 
Aaache huo ujinga ana mengi ya kufanya hasa kupatana na kizazi chake walioingia nap Rwanda mwaka 1994!

Kina kayumba nyamwasa na wengineo na atubu dhidi ya maumivu aliowasasbabishia!

Lah ivyo hatomaliza muhula wake wa urais Mungu hataniwi!
 
Anaingiza bunduki ndani ya nyumba za Ibada!!

Vita hiyo ni kubwa hatoiweza, ataishia kuliwa na chango kama farao,na habari yake itaishia Hapo.
 
Back
Top Bottom