Katika hili, namuunga mkono dikteta PK.
Na Tanzania nayo ipige marufuku kufungwa vipaza sauti juu ya nyumba za ibada, na hivyo kuwasababishia watu kelele. Iwe ni marufuku kufungulia mziki kwa sauti ya juu nyakati za usiku kwenye nyumba za ibada.
Wachungaji, manabii, mitume, na maaskofu wote lazima wawe na elimu ya teolojia.
Iwe ni marufuku kwa manabii/mitume kuwahadaa watu eti wanaponya ukimwi, kisukari, kansa, wanafanya miujiza ya kupata utajiri, nk. Huu ni utapeli wa wazi kabisa.