PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Kwa mara ya kwanza Rwanda imekiri kuwa inashirikiana na kundi la waasi wa AFC/M23 katika vita vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Balozi wa Rwanda nchini Marekani Mathilde Mukantabana ameiambia kamati ya Bunge la Marekani kwamba Rwanda imekuwa ikifanya hivyo kwa sababu za kiusalama lakini pia kuzuia kundi la wapiganaji wa kihutu la FDLR kuendesha mauaji ya jamii ya watutsi wa Kongo.
Hatua ya Rwanda kukiri uhusiano huu na kundi ambalo kwa muda mrefu imekuwa ikikanusha kuliunga mkono imezua mijadala na michango mseto kuhusu hatua hiyo ya Rwanda.
Katika tangazo lililotolewa na ubalozi wa Rwanda mjini Washington baada ya kikao cha balozi wa Rwanda nchini Marekani Mathilde Mukantabana na kamati ya Bunge la Marekani, Rwanda imekiri kuwa na ushirikiano na AFC/M23 katika utaratibu wa shughuli za kiusalama katika kuwalinda raia wa Kongo wenye asili ya Rwanda hasa wale kutoka kabila la Watutsi ambao tangazo hilo linasema wanaendelea kufanyiwa vitendo vya mauaji na unyanyasaji wa aina nyingine na makundi yenye silaha katika mzozo wa Mashariki ya Congo hasa kundi la wanamgambo wa kihutu la FDLR ambalo Rwanda inasema lilihusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Balozi wa Rwanda nchini Marekani amesema: "Ingawa Rwanda na AFC/M23 wanashiriki katika lengo la pamoja la kuwalinda Watutsi katika DRC dhidi ya wapiganaji wa FDLR na wanamgambo wengine wenye misimamo mikali wanaoungwa mkono najeshi la Kongo FARDC, maslahi ya nchi yangu yanakwenda mbali zaidi ya hilo: kuzuia kujirudia kwa uasi na mauaji ya kimbari yanayovuka mipaka, kama yale ya mwishoni mwa miaka ya 1990, ambayo yanaweza kutishia uwepo wa Rwanda yenyewe”
Lakini baadhi ya wananchi ambao hawakutaka majina yao kutajwa wamesema kauli ya serikali ya Rwanda imethibitisha yale madai ya muda mrefu ya serikali ya Kinshasa pamoja na Umoja wa Mataifa kuwa Rwanda inalisaidia kundi hilo. Jean Batiste Gasominari ambaye ni mwanasheria na mchambuzi wa siasa za Maziwa Makuu, anasema ushirikiano huo ni wa kimaslahi zaidi kuliko hali ya kawaida
Hata hivyo baada ya kauli hiyo ya Rwanda, hakujatolewa tamko la mara moja kutoka Marekani wala upande wowote huru. Lakini Rwanda imekuwa wazi na kusema kwamba haina mpango wa kuamua hatima ya kisiasa au kijamii nchini Kongo isipokuwa tu kulinda usalama na maslahi yake.
Hatua ya Rwanda kukiri uhusiano huu na kundi ambalo kwa muda mrefu imekuwa ikikanusha kuliunga mkono imezua mijadala na michango mseto kuhusu hatua hiyo ya Rwanda.
Balozi wa Rwanda nchini Marekani amesema: "Ingawa Rwanda na AFC/M23 wanashiriki katika lengo la pamoja la kuwalinda Watutsi katika DRC dhidi ya wapiganaji wa FDLR na wanamgambo wengine wenye misimamo mikali wanaoungwa mkono najeshi la Kongo FARDC, maslahi ya nchi yangu yanakwenda mbali zaidi ya hilo: kuzuia kujirudia kwa uasi na mauaji ya kimbari yanayovuka mipaka, kama yale ya mwishoni mwa miaka ya 1990, ambayo yanaweza kutishia uwepo wa Rwanda yenyewe”
Kauli ya Rwanda yapokelewa kwa hisia mseto
Kauli hiyo ya Rwanda imepokelewa kwa hisia mseto. Bonaventure Cyubahiro ambaye ni mwandishi wa habari mjini Kigali amesema "Mimi nimeona kilichofanywa na serikali ya Rwanda ni ukweli. Kwa sababu serikali ya Kongo inaendelea kuisaidia FDLR. Tumeona wanaendelea kuwaua Watutsi nchini Kongo, Wanyamurenge wakitawaja kama Wanyarwanda yaani ni kama mauaji yanaendelea."Lakini baadhi ya wananchi ambao hawakutaka majina yao kutajwa wamesema kauli ya serikali ya Rwanda imethibitisha yale madai ya muda mrefu ya serikali ya Kinshasa pamoja na Umoja wa Mataifa kuwa Rwanda inalisaidia kundi hilo. Jean Batiste Gasominari ambaye ni mwanasheria na mchambuzi wa siasa za Maziwa Makuu, anasema ushirikiano huo ni wa kimaslahi zaidi kuliko hali ya kawaida