Rwanda yalalamikia vikwazo vya Uingereza dhidi yake

Mateso chakubanga

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2021
Posts
587
Reaction score
800
Rais wa Rwanda Paul Kagame na serikali yake wamelalamikia vikwazo vilivyowekwa na Uingereza dhidi yake.

Serikali ya Rwanda imesema vikwazo vilivyowekwa na Uingereza kuihusu Rwanda baada ya kushutumiwa kuunga mkono machafuko nchini DRC kwa kutoa misaada ya kijeshi na zana kwa kundi la waasi la M23 sasa wameelewa Uingereza ipo upande upi hasa,

Aidha, vikwazo hivyo vitaleta mtikisiko katika serikali na wananchi kwa ujumla na kamwe watasimamia usalama wa raia wao na kutoogopa vikwazo ingawa vina madhara dhidi yao, msemaji wa serikali ya Rwanda Bi Yolande Makolo amesema wamepewa shutuma zisizo na ukweli juu ya kuunga mkono wanamgambo waasi wa M23.

Deutch Welle.(DW)

Formula ni moja tu ifanyike kura ya maoni ya raia waishio eastern province of congo kama wanataka kujitenga ama la.
Kwani kuna siku wananchi wa eastern DRC walilalamikia kuwa sehemu ya DRC? Makundi ya wahuni yavamie nchi kwa ufadhili wa nchi nyingine halafu wananchi waulizwe kama wanataka kujitenga au la? Hakuna referendum ya hivyo.
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame na serikali yake wamelalamikia vikwazo vilivyowekwa na Uingereza dhidi yake.

Serikali ya Rwanda imesema vikwazo vilivyowekwa na Uingereza kuihusu Rwanda baada ya kushutumiwa kuunga mkono machafuko nchini DRC kwa kutoa misaada ya kijeshi na zana kwa kundi la waasi la M23 sasa wameelewa Uingereza ipo upande upi hasa,

Aidha, vikwazo hivyo vitaleta mtikisiko katika serikali na wananchi kwa ujumla na kamwe watasimamia usalama wa raia wao na kutoogopa vikwazo ingawa vina madhara dhidi yao, msemaji wa serikali ya Rwanda Bi Yolande Makolo amesema wamepewa shutuma zisizo na ukweli juu ya kuunga mkono wanamgambo waasi wa M23.

Deutch Welle.(DW)

View attachment 3250648
Mabeberu piga spana huyo mvamizi.....mpaka RDF waondoke Bukavu na Goma

Tresor Mandala Hammaz
 
Siyo rahisi kiasi hicho. Kama ingekuwa ni rahisi kiasi hicho, kila mwaka yangekuwa yanazaliwa mataifa mapya. Hata Tanzania isingekuwepo.
Kama ulaya walikubali Ukraine ikamegwa na Urus kule Crimea basi hawana sifa ya kuzuia hayo huko Congo. Lakini pia Trump na wajinga wenzake wanasema Russia yupo sawa kuivamia Ukraine basi hata Rwanda afanye anavyoona ni sawa.
 
Kwani kuna siku wananchi wa eastern DRC walilalamikia kuwa sehemu ya DRC? Makundi ya wahuni yavamie nchi kwa ufadhili wa nchi nyingine halafu wananchi waulizwe kama wanataka kujitenga au la? Hakuna referendum ya hivyo.
Mkuu kwanini muhuni Putin anaonekana ni sawa kwake kuivamia Ukraine
 
Baada ya Uingereza kuikatia misaada Rwanda hivi punde kutokana na mauaji ya Halaiki huko Congo ili kuiba madini Hatimaye Uingereza imeungana na Ubelgiji kuiwekea kukata misaada Rwanda.
Rwanda ilijibu mapigo kwa ubelgiji kwa kuiwekea Vikwazo.

Inavodaiwa Vikwazo Lukuki vinakuja baada ya Marekani kuanza na viongozi wa M23
je inauwezo wa kuiwekea vikwazo pia uingereza.
 
Ngoja tuone ila Brussels sio ya kuiendea haraka haraka
Huenda kagame akakalia kuti kavu
 
Kama ulaya walikubali Ukraine ikamegwa na Urus kule Crimea basi hawana sifa ya kuzuia hayo huko Congo. Lakini pia Trump na wajinga wenzake wanasema Russia yupo sawa kuivamia Ukraine basi hata Rwanda afanye anavyoona ni sawa.
Dunia uwanja wa fujo
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame na serikali yake wamelalamikia vikwazo vilivyowekwa na Uingereza dhidi yake.

Serikali ya Rwanda imesema vikwazo vilivyowekwa na Uingereza kuihusu Rwanda baada ya kushutumiwa kuunga mkono machafuko nchini DRC kwa kutoa misaada ya kijeshi na zana kwa kundi la waasi la M23 sasa wameelewa Uingereza ipo upande upi hasa,

Aidha, vikwazo hivyo vitaleta mtikisiko katika serikali na wananchi kwa ujumla na kamwe watasimamia usalama wa raia wao na kutoogopa vikwazo ingawa vina madhara dhidi yao, msemaji wa serikali ya Rwanda Bi Yolande Makolo amesema wamepewa shutuma zisizo na ukweli juu ya kuunga mkono wanamgambo waasi wa M23.

Deutch Welle.(DW)

View attachment 3250648
Kagame na wazungu wanatufanyia maigizo
 
Hivi kwanini Kagame hatoki madarakani? amekua akitawala kwa miongo mingi je serikali yake ni kidikteta?
 
kwaio hata tz kungekuwa na madini kama congo kungekuwa na makundi ya kutaka uhuru wao si ndi
 
Tanzania kundi ni moja tu CCM lakini nao wanakoelekea tunaweza kuona wakigawanyika. Hawa bado wanakula na familia zao kwa kushirikiana.
 
Back
Top Bottom