Sijasema kila mmoja apimwe mjadala ulikua umuhimu wa kua na test kit.Sio kweli unavyosema, testing hufanywa kwa mtu mwenye kuonyesha dalili pekee, kama hana dalili hafanyiwi testing, anachofanyiwa ni kuwekwa chini ya karantini kwa siku 14 kama ataonyesha dalili, na katika kipindi hicho cha karantini, haruhusiwi kuchanganyika na watu, hivyo sio sawa ukisema kwamba mtu ambaye hahapimwa anahatarisha watu wengine.
Kaka lazima ukubali kwamba, kama ugonjwa haujaingia nchini, nguvu lazima ziwekwe katika "Screening not testing", ukishaanza kuzagaa ndio testing inaanza kuwa muhimu. Kwanza itaanza katika maabara moja nchi nzima, kadri ugonjwa unavyoeenea ndio umuhimu wa kueneza sehemu za kupima nchi nzima unapojitokeza. Hapo Kenya ni sehemu moja tu ndio inapima Corona, kwanini usiwashauri wasambaze vipimo nchi nzima kwa sasa?, jibu ni kwamba kwasababu bado ugonjwa haujafika nchi nzima. Prudent use of public resourses.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhusu kuhatarisha wengine... mfano umepima joto la mtu likawa juu ukampeleka karantini, labda ana flu. baadae ukampima mwingine joto lake likawa juu, nae ukampeleka karantini pamoja na yule wa kwanza. chances are yule wa kwanza ataambukizwa na huyu wa pili.