Rwanda yazindua taxi za umeme za angani zinazoruka bila rubani

Rwanda yazindua taxi za umeme za angani zinazoruka bila rubani

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Rwanda imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza barani Afrika katika kuendeleza teknolojia ya usafiri wa anga, kupitia mipango ya kutumia taxi za angani zinazotumia umeme na zinazoweza kuruka bila rubani.

Teknolojia hiyo, inayojulikana kama Electric Vertical Take-Off and Landing (eVTOL), inaruhusu ndege ndogo kupaa na kutua wima bila kuhitaji uwanja mkubwa wa ndege, huku baadhi ya mifumo yake ikiwezeshwa kufanya safari kwa kutumia teknolojia ya kujiendesha yenyewe.

Taxi hizo za angani zina uwezo wa kusaidia kupunguza msongamano wa magari mijini, kurahisisha usafiri na kupunguza utegemezi wa magari yanayotumia mafuta.

Rwanda inadaiwa kuwa ndiyo nchi ya kwanza na pekee barani Afrika kuzindua huduma hiyo ila madai hayo yanapigwa na baadhi ya watu.

Teknolojia hii inaweza kuwa hatua muhimu katika mustakabali wa usafiri barani Afrika, huku Rwanda ikijitahidi kuimarisha nafasi yake katika ubunifu na matumizi ya teknolojia za kisasa.

FB_IMG_1791921568484.jpg
 
Testing the microphone another Chivayo incident i repeat another Chivayo incident
 
Taxi hizo za angani zina uwezo wa kusaidia kupunguza msongamano wa magari mijini, kurahisisha usafiri na kupunguza utegemezi wa magari yanayotumia mafuta.
Zikiletwa TZ zitaua sana, tazama vifo vinavyosababishwa na bodaboda na magari
 
Kabla hujaleta hizo korokocho ili ujipatie ujiko unapaswa ujiulize

Huko waliko zibuni wanazitumia kwa asilimia ngapi?
 
Back
Top Bottom