Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwenyekiti wa Chemba ya Wachimbaji madini Tanzania, Mhandisi Filbert Rweyemamu amesema shughuli za uchimbaji wa madini nchini haziwezi kuanza bila kufuata sheria kuu nne zinazolinda masilahi ya wananchi na mazingira.
Amesema sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Uhifadhi Mazingira ya mwaka 2004, Sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 inayosisitiza ushirikishwaji wa jamii na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 ambayo inalinda haki za wananchi katika umiliki wa ardhi.
“Kwa maana nyingine hakuna uchimbaji wa madini utakaoanza Tanzania bila kupitia ngazi zote hizi, ikiwa ni pamoja na kushirikisha jamii husika,” amesema Rweyemamu.