Kabaridi, walipwa na TNA?lol.. Mtazamo wa wakenya kwa muungano wa TNA unashawishiwa na vitu vitatu;
kwanza ni sera za ugavi wa mamlaka kati ya TNA na URP ambayo ni ile ya nusu mkate, asilimia 50 kila upande jambo ambalo limewafanya hawa wenzetu wawili kuwa vigogo wakuu. Hebu tujikumbushe mtazamo wa wakenya kwa viongozi wao, weka kabila langu serikalini na pia mimi nipo serikalini. Sivyo? Wao walihubiri sana TNA/URP wakasahau uongozi jumilifu ingawa baadaye waliongeza kina Balala, Ongeri na the likes but mtazamo haujabadilika sana kwa mkenya .
Pili, Kenya imekuwa na viongozi watatu; mkikuyu na mkalenjin. Kwa kadri flani, wakenya wameshachoka. Mbona tusijaribu kigogo mwingine, laiti tu asiwe wa Mlima Kenya? Waelewa? Si eti taswira na sera za CORD ni kuhusu arubaini na moja dhidi ya moja. LA!!! Sisi kama wakenya ndio tumechoka, twataka mabadiliko endelevu kaka. uongozi wa nchi hauezi chezea eneo moja au mbili kila uchao. By chance it happens that the incumbent president is from central province and of which to me is alil counterproductive for one Uhuru Muigai.
La mwisho ni kwa waathiriwa wa uchaguzi, donda lipo bado, na kama halipo, nafsi yakataa. Wosia wangu ni huu; ni vema hawa wawili wakajinadhifishe kwa kina kule wanakohitajika kabla ya kukwea madarakani. Na kama hawawezi, natumai wakenya watakubali kuishi na mshikomshiko wa kiuchumi kama vile Sudan na nchi zinginezo zilizotengwa.
Ni hayo tu kwa sasa na si ukabila, sina ukoo na Raila, Uhuru ama Ruto. Naitamania tu nchi ya Kenya yenye mabadiliko mema na uongozi mwafaka. Si purukushani za kimataifa kila wakati kujaribu kutakasa ovu lililotendeka. CORD yaimarika, asilimia 51 ya wakenya wanadhania hivyo kulingana na kura za maoni.