Saa 48 ngumu kwa wachezaji Simba!

Akanywe naye chai nyumbani kwake lakini sio kuwa kwenye squad
Ntibazonkiza ni mfungaji bora wa msimu uliopita! Halafu mnamkataa hata kabla ya msimu wa ligi kutamatika!!

Mshasahau kwenye mechi moja tu na polisi Tanzania alitupia goli 5!! What a bull striker!! Mimi nitashangaa sana kama Mwenyekiti Mangungu atazisikiliza hizi kelele zenu.
 

Hii ndio nataka sasa. Huwezi kuwa na timu ya wapambe na viongozi. Fyeka fyeka kabisa.. naanza mimi, hawa wachezaji wa njee hawastahili tena kuvaa jezi ya simba

1. Chama
2. Phiri
3. Baleke
4. Onana
5. Saido

Ndani punzisha Boko akina kapombe, Mohamed wapate mbadala , Israel apewa nafasi zaidi ni bonge mmoja la fullback .


Huwezi shindana CAF na wachezaji hawa kamwe. Ondoa kabisa anza upya, sajili nguvu sana vunja benki then mpe Benchika muda .. Al Ahly na mapesa yake anapigwao
 

Umeweka vyema sana ila Phiri umri unamkataa kabisa limebaki jina tuu.. umeweka safi kabisa hapo kwenye uangalizi ila phiri atupishe tuu
 
Niliwaambia onana alicheza ligi ya Rwanda haina nguvu kama ligi yetu .. ni kawaida saana.. mpaka sasa simba hatuna mshambuliaji kiongozi ambae anaweza fungu eneo lolote au eneo gumu kama alivyokuww Mayele.. we need bully striker hata 2
 
Kocha anaboresha kikosi kwa kuangalia uwezo wa mtu wa sasa. Saido ni mzuri ila muda umemtupa mkono. Ni kati ya watu wanaopewa nafasi kubwa sana kwa sasa lakini hawajaonyesha makali. Wawapishe wengine
 
Sasa hapo si una anza upya
 
Mchukueni nyie
 
Namkubali sana huyu kocha. He’s the real boss. No nonsense.

Hata nidhamu ya wachezaji ipo juu. Mfano Putin amebadilika kabisa anamuogopa kama baba yake😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…