Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Hotuba za mkuu wa Mkoa wa Kagera zinajaa aina fulani ya ucheshi na ni wa kipekee. Huwa ni wa kwake mwenyewe haufanani na wa mwanasiasa mwingine yoyote. Maongezi yake yanafikirisha lakini yanawekwa hadharani kwa njia ya kuchekesha.
Wapo wanaodhani kuwa ameupata ukuu wa Mkoa kama bahati tu, kama zali tu. Wapo wanaojua namna watu wa vitengo wanavyopatikana tangu wakiwa mashuleni. Darasani mnakuwa na mwanafunzi mmoja na hamuwezi hata kumtarajia kuwa ni mtu wa mfumo, kumbe tayari ameshachukuliwa na anafanya kazi maalum kisirisiri.
Wanasiasa ni watu wenye utayari wa kufanya mambo ambayo wasio wanasiasa wanajionea uzito sana kuyafanya. Kule kuwa tayari kujikomba mbele za watu huku ukimpamba Mwenyekiti wa Chama kama vile ni malaika aliyeshuka kutoka mawinguni kunahitaji ujasiri usioweza kuongelewa ukaeleweka.
RC wa Kagera Albert Chalamila amekuja na kauli inayofikirisha akihutubia katika shughuli fulani aliyokuwa mgeni wa heshima huko Kagera. Kawasema waheshimiwa wanaoutaka urais wakiwa bado ni mawazri. Watoto wa mjini wanasema 'kajilipua'. Kwamba waziri anatumwa kikazi Ulaya halafu anaanza kukusanya pesa za kampeni ya kuelekea 2025 uchaguzi.
Ni huyu RC aliyewekwa pembeni baada ya kupishana kauli na aliyempa ukuu wa mkoa wa Mwanza hivyo leo kuwa mtetezi wa bosi wake licha ya kuwa ni haki yake lakini ni uamuzi wenye kufikirisha kidogo.
Je anajivuta karibu na kambi ya SSH kama mwanasiasa anayemtumikia kafiri apate mradi wake?. Je alikuwa team mmoja na rais wa sasa kwa kipindi kirefu hivyo ametumwa na bosi wake ili awachambe mawaziri wanaodhani kuwa hii ni awamu ni ya kwao kupeta?.
Au kauli ile ni ya kimkakati zaidi, ionekane kuwa SSH hana makundi ila yeye anashughulika na maslahi ya kitaifa mwaka huu wa 2022 ikiwa ni miaka mitatu kabla ya uchaguzi wa 2025?. Usimwamini mwanasiasa hata sekunde moja lakini pia usimwamini yule anayemtuma mwanasiasa na kuwa ndio sababu ya kupoteza ile aibu ya asili tena mbele za watu.
Namchukulia Albert Chalamila kama saa mbovu (mapepe/chakaramu) muda wowote ule anajilipua bila ya kujali. Lakini huyu pengine ni saa mbovu kwa maana halisi kwamba kuna muda unafika inasema ukweli licha ya kila mtu kuujua ubovu wake.