Saa moja na dakika 17

Fundi manyumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Posts
3,799
Reaction score
8,063
Wakuu habari za mda huu.

Natumai wote wazima na tunaendelea vizuri na majukumu yetu.

Hata hivyo mi mzima japo jana mida ya saa 4 usiku nilikutana na changamoto ambayo imenifanya nije hapa kuwapa tahadhari wenzangu.

Wanasema haya mambo hayamkuti nyani.

Kama mimi jana yalinikuta basi hata wewe kesho yanaweza kukukuta.

Wakuu naongea haya na maanisha wakuu namaanisha shika haya nayosema.

1- Epuka kula ngano(skonzi,mkate)

2- kunywa maji ya kutosha

3- Ukihisi haja nenda mda huo huo


Wakuu hivo vipengele hapo juu najua mmesoma fasta fasta ila nakuomba rudia maana hii hali inapokufika unakua wewe peke yako.

Jamani tunywe maji.Wanaposema maji ni muhimu kwa mwili wa binadamu hawajakosea jama..

Kilichonitokea mimi jana naapa sitojihusisha tena na kula ngano..(dry mkate) wakuu mara kumi unywe maji ulale tuu ila ngano (ney)

Mpaka sasa nipo hai nashukuru Mungu alhamdulillah maana ile kitu lisaa limoja na dakika 17 napambania ,,hapana mpka nimetoka mzima naimani mungu ana makusudio yake.
Asanteni.

Maji ni muhimu kwa binadamu.. ninyime mkate nipe maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…